Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema.
……………………………………………………..
Na Heka Wanna na ShakilaGalus,MAELEZO
MATUKIO
ya uhalifu nchini yameonyesha kupungua kutokana na ushirikiano mzuri
baina ya wananchi kwa kutoa taarifa za uhalifu kwa jeshi la polisi.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP), Isaya Mnguru alisema kuwa kwa kipindi cha kuanzia Januari
hadi Novemba, 2012 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2011
takwimu zinaonesha hali ya uhalifu imepungua.
Aidha
kumejitokeza na matukio kadhaa ya makosa dhidi ya kuania mali,makosa
dhidi ya binadamu, makosa dhidi ya maadili na makosa dhidi ya usalama
barabarani.
DCP
Mnguru alisema kuwa hali ya mwenendo wa uhalifu kwa mwaka 2012 makosa
makubwa ya jinai yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi ni 66,255
ikilinganishwa na makosa 69,678 yaliyo ripotiwa kwa kipindi cha mwaka
2011 ni upungufu wa makosa 3,423 ambao ni sawa na 4.9%.
Aliendelea
kuwa takwimu zinaonesha matukio makubwa ya usalama barabarani
yaliyoripotiwa ni 21,531 ikilinganishwa na matukio 22,208 yaliyoripotiwa
mwaka jana ambapo ni upungufu wa matukio 677 ambao ni sawa na 3%.
Mnguru
alisema kuwa matishio ya usalama nayo yamepungua kwani mpaka sasa hivi
hakuna tishio la dhahiri hapa nchini kuhusiana na tishio la ugaidi.
Alisema
hali hiyo imetokana na hatua zilizochukuliwa katika kuimarisha ulinzi
kwenye mipaka na maeneo nyeti sambamba na kuwatahadharisha wananchi kuwa
waangalifu na kutoa taarifa za nyendo za watu au vikundi wanavyovitilia
mashaka.
Aliongeza
kuwa jeshi la polisi linaendelea kubuni na kutekeleza kikamilifu
mikakati ya kukabiliana na uhalifu ikiwemo kushirikiana na wadau wote wa
ulinzi na usalama katika kubadilishana taarifa za kiintelijensia pamoja
na uzoefu wa kuzuia uhalifu kwa kuibua mifumo mipya na kuboresha ya
zamani.
Alisema
namba za simu za makamanda wa polisi zimesambazwa nchini kote
wananchi wasisite kuzitumia wapoona viashiria vya uhalifu. aliwaonya
wale wote wasiopenda kutii sheria kwa hiari yao kuacha tabia hiyo
wakiemo madereva wa mabasi ya abiria kutotii sheria za barabarani pamoja
na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kutovaa kofia ngumu na
kupakia abiria zaidi ya mmoja.
0 comments:
Post a Comment