Bodi
ya Wakurugenzi ya Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) imepiga
kura kumruhusu bondia wa Tanzania Fadhili Majia apambane na bondia
wa Ghana katika mchujo (Elimination) wa kutafuta mpinzani atakayekutana na bingwa wa mkanda wa Jumuiya ya Madola katika uzito wa Fyweight Kevin Satchell wa Uingereza. Mpambano wa Fadhili Majia na Isaac Quaye utafanyika jijini Accra, Ghana tarehe 22, Febryary 2013.

Rais
wa TPBC Onesmo Ngowi ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya Baraza la Ngumi
la Jumuiya ya madola na alikuwa wa kwanza kumpigia bondia Fadhili Majia
kura ili acheze na Quaye.
Hii
itakuwa mara ya kwanza kwa bondia Fadhili Majia kugombea mkanda wa
Jumuiya ya Madola ambayo inaziunganusha nchi zote zilizokuwa
zinatawaliwa na himaya ya Kiingereza.
Wakati
huo huo Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola
imepitisha azimio la kuruhusu ubingwa wa baraza hilo katika bara la
Afrika. Ubingwa huo utakuwa unajukikana kama “CBC Africa Zone” na tayari
wapo mabondia kadhaa wa nchi za Afrika ya Magharibi ambao wameshandaa
mapambano mwakani.
Napenda
kuwahamasisha mapromota wa Kitanzania kuchangamkia fursa hizi adimu na
kuandaa mapambano ya ubingwa wa “CBC Africa Zone” kwa manufaa ya
mabondia wetu.
TPBC
imejiandaa kuwatafutia mabondia wa Kitanzania mapambano mengi ya nje
ili waweze kujijenga kimchezo na pia kuweza kupata kipato kizuri.
0 comments:
Post a Comment