Mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi akihutubiwa wananchi wake.
Viongozi
wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi na Momba wametakiwa kuhakikisha wanafuatilia
kero ya muda mrefu ya wafugaji wanaoishi pembezoni mwa ziwa Rukwa kutozwa faini
pasipo kupewa stakabadhi.
Hayo
yalisemwa na mbunge wa jimbo la Mbozi magharibi DEVID SILINDE wakati wa
mahojiano na Bomba Fm kuhusu sakata hilo na kuongeza kuwa endapo uongozi wa
Serikali hautoweza kulifuatilia suala hilo wananchi watagoma kuchangia fedha
hizo ikiwa ni pamoja na fedha nyingine za maendeleo.
Alisema
tatizo hili la faini kiholela limekuwa mtaji kwa watu na viongozi wote wa
halmashauri na wilaya wamekwisha fikishiwa taarifa kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi
wa tatizo hilo.
“Kwa
sasa tumetoa kipindi hiki cha sikukuu kwa viongozi wa hlamahauri kuhakikisha
tatizo hilo wanalimaliza na vinginevyo tutahamaisha wananchi wasishiriki hata
kidogo katika shughuli za maendeleo kwani wamekwisha nyonywa vya kutosha.”alisema
Silinde
Wakati
huohuo alitoa wito kwa wakazi wa wilaya ya Momba kujitokeza kwa wingi katika
kuchangia harambee ya kuchangia upatikanaji wa huduma ya maji na elimu ambapo
harambee hiyo itahudhuriwa pia na wabunge mbalimbali hapa nchini
“Harambe
hiyo imelenga kutafuta ufumbuzi wa tatizo Sugu la maji na elimu katika
halmahaur yetu ya mji wa Tunduma na wilaya ya Momba kwa ujumla” alisema Silide.
Kuhusu
tatizo la njaa jimboni mwake amesema hatua za haraka zimeanza kuchukuliwa kwa
kusambazwa kwa chakula katika kata na kaya zinazokabiliwa na tatizo hilo
wanapatiwa chakula
“Hakuna
tatizo la njaa kwa wananchi kwa sasa kwani hatua zimeanza kuchukuliwa na hadi
sasa tumekwisha gawa mahindi kwa kila kata inayokabiliwa na matatizo hayo ambapo
zoezi la usimamizi wa chakula hicho limekabidhiwa kwa madiwani kwani wao ndio
wenyeviti wa kata”.
0 comments:
Post a Comment