Pages

Home » » MWAKEYEMBE AZIDI KUHIMARISHA USAFIRI WA RELI NCHINI, SASA TRENI KWENDA MWANZA NA MOSHI

MWAKEYEMBE AZIDI KUHIMARISHA USAFIRI WA RELI NCHINI, SASA TRENI KWENDA MWANZA NA MOSHI

 Gari moshi likikaribia kufika stesheni ya Mwanza

Jengo la Shirika la Reli Mwanza
Tangazo likionyesha kuanza kwa safari za gari moshi

Abiria wakishuka baada ya gari moshi kufika steshen ya mwanza

Raia wa kigeni nao walikuwa miongoni mwa abiria waliowasili na gari moshi

Waandishi wa habari wakizungumza na naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizeba

Moja ya mabehewa ya Gari Moshi

Wananchi waliofika kushuhudia kufika kwa gari moshi kwenya stesheni ya mwanza

Moja ya behewa la gari moshi likiwa katika hali mbaya

Naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizebaakitoka kuzindua safari za gari moshi

Salamu kwa Dk Mwakyembe
Shikamoo Dk  Mwakyembe, habari ya Jumapili najua utakuwa umepumzika leo jumapili baada ya majukumu ya wiki iliyopita , mimi rafiki yako Mkami Jr baada ya kutoka kukusaidia kazi ya kukagua Reli ya Moshi, Nimeamua nisafiri mpaka kanda ya ziwa  nikusaidie tena kazi ya kukagua.

Dk Mwakyembe najua utashangaa kwanini nimejipa kazi hii bila kupewa kibali cha ofisi yako (Wizara ya uchukuzi), binafsi mimi nimejiajiri kufanya kazi zote za umma hivyo nadhani hata kazi hii ya kuja mwanza kukagua reli ni moja ya majukumu yangu kama mfanyakazi wa umma nisiye na ofisi wala mshahara au posho ya safari Dk mwakyembe usije shangaa siku nyingine nikafika hadi bandarini nikusaidie kupunguza msongamano wa makontena kwa kazi hizi nazofanya sihitaji kusifiwa, sihitaji posho ila nimeipenda tu kazi hii.

Dk Mwakyembe kama ambavyo niliyoona hali ya reli kule Moshi ambapo nilikuta Reli na majengo mabovu na behewa moja tu na sikuona dalili zozote za reli ile kufanya kazi na wala sikuona matumaini kama kuna siku itafanya kazi.

Leo hii Dk Mwakyembe umeniwahi huku Mwanza  sina budi kukupongeza wewe na timu yako kwa kazi nzuri kazi nzuri mnayofanya, leo nimeona Gari moshi likifika stesheni ya Mwanza na nimeomuona Naibu Waziri wako Dk  Dk. Charles Tizeba akizungumzia ujio wa safari za Gari moshi huku akisema maneno yenye kutia matumaini ikiwemo kuboresha usafiri huo kadri uwezo unapopatikana ni maneno ya faraja naamini amezungumza kwa niaba ya ofisi yako hivyo nawe unahusika kutekeleza aliyoyasema msaidizi wako, 
Pamoja na sifa ambazo wananchi wanakumwagia ila Rafiki yangu Dk Mwakyembe kazi ngumu ipo mbele yako ndio maana nikaona nikusaidie baadhi ya mambo , Jambo kubwa ambalo wananchi wamekuwa wakizungumzia usafiri huu ambao kwao ni ukombozi ni jambo la kuhujumiwa , mfano leo nimesikia kuwa wenye mabasi hutumika kuhujumu miundombinu ya reli na kufanya gari moshi kusimama kufanya kazi mara kwa mara, Sina ushahidi kuhusiana na jambo hili ila waswahili walisema lisemwalo lipo kama halipo laja..
Nikutakie kazi njema Dk harrison Mwakyembe na msaidizi wako  Dk. Charles Tizeba  na timu yako ya wizara ya uchukuzi na timu nzima ya Shirika la reli kwa kazi nzuri mnayoifanya ila inabidi mjipange kukabiliana na changamoto ikiwamo hujuma katika miundombinu na kuboresha magari moshi hapa nikiwa na maana kukarabati injini za gari moshi na kukarabati mabehewa yawe ya kisasa zaidi. 
Asante sana Dk Mwakyembe nikutakie mapumziko mema ya weekend na fikisha salamu  zangu kwa familia yako bila kumsahau dereva wako na kesho ukiwa ofisini fikisha salamu zangu kwa Katibu Muhtasi wako hawa ni watu muhimu pia kwenye kazi yako
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger