Pages

Home » » POLISI WATANGAZA VITA KWA MADEREVA WASIOFUATA SHERIA BARABARANI MBEYA

POLISI WATANGAZA VITA KWA MADEREVA WASIOFUATA SHERIA BARABARANI MBEYA

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI

Na.Mwandishi wetu

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMAN amesema jeshi la polisi limekuwa likilazimika kutumia shuruti kwa madereva wa daladala kutokana na madereva hao kutofuata sheria zilizopo.

Akiongea na mwandishi wetu kamanda ATHUMAN amesema mamlaka ya kudhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) hawatasita kuwachukulia hatua madereva wazembe.

“Kila mtu anatakiwa kufuata sheria na mtu yeyetote ambaye atafanya kosa asitegemee kama atasamehewa kwa uzembe wake, na kwa mtu yeyote ambaye atakatisha ruti hatua kali za kisheria, pia wamilikiwa wa magari wahakikishe madeeva wao wanafuata utaratibu ikiwa ni pamoja kutopandisha nauli kwa daladala ziendazo Mbalizi na ruti kuishia Sae badala ya uyole Dereva atachukuliwa hatua mara moja bila huruma yoyote”Alisema Kamanda ATHUMAN.

Wakati huohuo amewataka wakazi wa mkoa wa Mbeya kutojihusisha na vitendo vya vurugu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi dhidi ya wote ambao wanahatarisha amani ya nchini

“Usalama ni eneo muhimu la kulipa kipaumbele endapo tutakuwa tumedhamiria kufikia malengo yetu katika shughuli mbalimbali, pia vitendo vya vurugu vinakwamisha maendeleo kwa wawekezaji kuingiwa na hofu ya kuwekeza mkoani hapa”

Kuhusu suala la askari kulazimisha madereva kutoa rushwa barabarani amesema dawa imekwisha patikana na tatizo hilo linaweza kumalizika kwa ushirikiano kati ya Jeshi lake, wananchi na waandishi wa habari

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger