Pages

Home » » SERIKALI KUONGEZA UDAHILI WA WANAFUNZI SEKTA YA AFYA

SERIKALI KUONGEZA UDAHILI WA WANAFUNZI SEKTA YA AFYA

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Dar es Salaam

Serikali inatarajia kuongeza udahili wa wanafunzi wanaosomea masomo katika sekta ya afya nchini kutoka wanafunzi 7500 hadi 10,000 kwa mwaka ifikapo 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wadau wa chanjo barani Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema udahili huo utasaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi katika sekta hiyo.

Waziri Mwinyi amesema uhaba wa wafanyakazi katika sekta ya afya umesababisha kutowafikia watoto wote nchini ili kuwapatia chanjo za magonjwa mbalimbali.

Kwa upande wake muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa Tanzania, Lufaro Chatora amesema shirika hilo likisaidiana na Wizara ya Afya wanafanya jitihada ya kuongeza magari ili kuwafikia  wototo wote na kuwapatia chanjo.

Mkutano huo wa siku tatu unawakutanisha wadau 200 wa huduma ya chanjo kutoka nchi mbalimbali barani afrika ambapo pamoja na mambo mengine watajadili jinsi ya kuboresha na kuimarisha  huduma ya chanjo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger