Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu akielekezwa jambo na ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Norbert Mtega. |
Jengo la utawala ambalo bado halijaanza kutumika |
Jengo la hosteli ya wanafunzi ambalo bado halijaanza kutumika
|
Serikali
imepongeza uamuzi wa Chuo Kikuu cha Mt Augostino Tanzania kuanzisha
kitivo cha udaktari katika kituo chake cha Songea. Hayo yalisemwa jana
tarehe 15.12.2012 na Mkuu wa
mkoa wa Ruvuma ndugu Said Thabit Mwambungu alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya chuo hicho kilicho katika eneo la Peramiho. Amesema
kuanzishwa chuo hicho ni ukombozi kwa Mkoa wa Ruvuma ambao awali haukuwa
na vyuo vya elimu ya juu.
“Kuanzishwa
kwa chuo cha Tiba ni lulu kwa mkoa wa Ruvuma kwa vile kitapunguza
usumbufu kwa wananchi wa ukanda huu ”alisema Mwambungu.
Aidha,
akijibu risala ya chuo kuhusu tatizo la ardhi kwa ajili ya upanuzi wa
eneo la chuo, Mwambungu amewataka watendaji walio chini yake wakae na
uongozi wa chuo kwa ufumbuzi. Alisisitiza kuwa anaamini liko ndani ya
uwezo wao.
“Watendaji kuanzia kijiji kaeni na viongozi wa chuo kupata ufumbuzi wa tatizo hili nanaamini hata likiwashinda, ofisi ya Mkuu wa Wilaya itawasaidia” alisema ndugu Mwambungu.
Akizungumzia
tatizo la maji, amekemea tabia ya wananchi kuharibu mazingira na vyanzo
vya maji na kusababisha tatizo la maji. Amewataka wananchi waache tabia
hii mara moja. Akifafanua zaidi amewataka viongozi wa dini waisaidie
serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tatizo la uharibifu wa
mazingira na athari zake.
“Nawaomba
viongozi wa dini mzungumze na waumini wenu kuhusu tatizo hili wakati
serikali inasimamia sheria kuhusu waharibifu na uharibifu mazingira”
Alisema Mwambungu.
Kwa upande wa umeme alisema watakaa na pande zote zinazohusika ili kupata ufumbuzi kwa vile linaigusa serikali pia.
Awali
mratibu wa Kitivo cha Udaktari Peramiho Chuo cha Mtakatifu Agustino
Tawi la Songea Padre Dunstan M. Mbano alisema Padre Mbano alisema chuo
kina wanafunzi 39 wa mwaka wa kwanza wanaosoma masomo ya udaktari ambao
wamelazimika kupelekwa kwa muda katika Chuo cha Ifakara-Morogoro kilicho
chini ya Chuo Mama
cha Mtakatifu Augustino wakisubiri kukamilika kwa miundo mbinu.
Alisema, hata hivyo, wanafunzi hawa kiutawala bado wako chini ya Chuo
Kikuu cha Mt Augustino Kituo cha Songea. Alisema Kituo cha Songea
kilizinduliwa Novemba mwaka 2011 na kina jumla ya wanafunzi 631.
Wanafunzi wa shahada ya kwanza ualimu kwa mwaka wa kwanza na wa pili ni
592 na wanaosoma udaktari ni 39.
Padre
Mbano alisema ujenzi wa chuo umegawanyika katika awamu tatu. Awamu ya
kwanza ilihusu ukarabati wa majengo ya iliyokuwa hospitali ya wakoma,
nyumba ya Mkuu wa Chuo, jengo la utawala na hostel kwa ajili ya
wanafunzi. Awamu ya pili na tatu zitahusisha ujenzi wa hostel mbili,
ukumbi, maktaba, ,adarasa na nyumba za walimu.
Padre Mbano alisema chuo kinakabiliwa na changamoto za ukosefu wa umeme, maji na samani na vifaa vya kufundishia. Kuhusu umeme, alisema zinahitajika shilingi za Kitanzania milioni 178.3 kuufikisha umeme katika eneo hilo na kwa upande wa samani na vifaa vya kufundishia zinahitajika shilingi za Kitanzania milioni 57.3.
0 comments:
Post a Comment