Pages

Home » » TAKUKURU MBEYA WAJICHIMBIA MAHAKAMANI NA MABARAZANI

TAKUKURU MBEYA WAJICHIMBIA MAHAKAMANI NA MABARAZANI

KULIA NI KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA MBEYA DANIEL MTUKA. (PICHA NA MAKTABA YA KALULUNGA blog)

* Wanasa wawili
 
VIKOSI vya taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mbeya vimeamua kujichimbia katika Mabaraza ya kata na Mahakama za Mwanzo kwa ajili ya kusaidia wananchi wanyonge wanaoombwa rushwa na watendaji wa vyombo hivyo, imebainika.

Akithibitisha kupeleka vikosi hivyo katika ngazi hizo za maamuzi na haki, Kamanda wa Takukuru mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka, alisema kuwa zoezi hilo limeanza kuzaa matunda ambapo tayari baadhi ya watendaji hao wamenaswa na Rushwa.

Mtuka alisema kuwa baada ya kupata malalamiko na taarifa kutoka kwa wananchi, taasisi yake ilipeleka maafisa wake na kuwaonya wale ambao hawakukutwa moja kwa moja na tuhuma na kuwakamata waliobainika.

''Mfano mzuri ni kule Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini ambako tayari tumewakamata Mwenyekiti wa Baraza la kata ya Nsalala na katibu wake ambao waliomba rushwa ya Sh.73,000 kutoka kwa mwananchi aliyekuwa akihitaji nakala ya mwenendo wa kesi yake ili akate rufaa'' alisema Mtuka.

Alitanabaisha kuwa mnamo Novemba 26, mwaka huu, mwananchi Ahadi Ndile ambaye ni Mkulima alitoa taarifa Takukuru za kuombwa rushwa na viongozi hao wa Baraza la kata baada ya kuhitaji nakala ya mwenendo wa kesi ya mgogoro wa ardhi/mipaka dhidi yake na Monica Ndeguha.

Baada ya taarifa hiyo Takukuru waliweka mtego ambao ulizaa matunda Desemba 4, mwaka huu baada ya mtuhumiwa Mwalimu mstafu James Mpalaza ambaye ni katibu wa baraza hilo na ni kiongozi wa Chadema na Asia Mwanyerere ambaye ni Mwenyekiti wa baraza hilo kupokea Rushwa ya kiasi hicho mali ya Takukuru.

Alisema kitendo walichokifanya watuhumiwa hao ni kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kifungu cha 15 cha mwaka 2007.

Watuhumiwa hao tayari wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya Desemba 5, mwaka huu na kupewa dhamana ambapo Kamanda Mtuka amesema kuwa mwisho wa kutamba kwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na mabaraza hayo ya kata wanaojifanya miungu watu kwa kuomba Rushwa kwa wananchi umefika.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa mara moja Takukuru wanapoombwa rushwa na watoa maamuzi au haki pia amesema kuwa Mamlaka zinazosimamia Mabaraza ya kata zinapaswa kuwajibika ipasavyo katika kuwasimamia watendaji wake ili kuondokana na malalamiko ya wananchi.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger