Pages

Home » » WILAYA YA MLELE KUWA NA HALMASHAURI MBILI – WAZIRI MKUU

WILAYA YA MLELE KUWA NA HALMASHAURI MBILI – WAZIRI MKUU

 

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi itakuwa na Halmashauri mbili za Mlele na Nsimbo ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo janamchana (Jumamosi, Desemba 15, 2012), wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Inyonga kwenye viwanja vya shule ya msingi Inyonga akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.

Aliwaeleza wakazi hao kwamba Rais Jakaya Kikwete aliamua kuwapa wilaya mpya na mkoa mpya kwa ili kuleta maendeleo kwa haraka. “Rais Kikwete alifanya hivyo kwa sababu alijua kwamba rasilmali zikiletwa Rukwa (mkoa wa zamani) hadi zifike hapa Mlele zitakuwa ni kidogo sana,” alisema.

Kufuatia mgawanyo huo, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele itakuwa na kata 13 ambazo ni Ilunde, Ilela, Nsenkwa, Inyonga, Utende, Kasanga na Mamba. Nyingine ni Majimoto, Mwamapuli, Mbede, Usevya, Itenka na Kibaoni.

Nayo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo itakuwa na kata 11 ambazo ni Ugalla, Uruira, Kasokola, Mtapenda, Nsimbo na Sitalike. 
Nyingine ni Kapalala, Machimboni, Litapunga, Itenka na Magamba. Ili kuendana na kasi ya mabadiliko, Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao wachangamkie fursa zilizopo kwa kuachana na kilimo cha matuta.
  Aliwataka mabwana shamba waandae mashamba-darasa kwa kila kijiji ili wananchi waweze kujifunza kwa mifano. Wakati huohuo, Waziri Mkuu ameahidi kutoa miche 1,000 ya miembe ya kisasa kwa vijana wa vijiji vya Uruira na Usense wilayani Mlele kama njia ya kuwahamasisha walime mazao mbadala.

Alitoa ahadi hiyo jana jioni (Jumamosi, Desemba 15, 2012), wakati akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo kwenye viwanja vya shule ya msingi Uruira katika kata ya Uruira wakati akiwa njiani kurejea Mpanda mjini.

“Nimemwambia Mkuu wa Mkoa (Dk. Rajab Rutengwe) ahamasishe kilimo cha maembe ya kisasa… yale ni makubwa ili muachane na haya madogo ya kwenu. Vijana hawa wapeni eneo nami nitawaletea miche 1,000 ya maembe ya kisasa kwa kuanzia,” alisema.

Akihimiza kanuni bora za kilimo, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mlele aliwataka waachane na kilimo cha matuta na badala yake watumie kilimo cha sesa. “Ekari moja ya mahindi inapaswa iwe na miche 16,000 ili ikupatie magunia 20-25 ya mahindi, sasa wewe unalima ekaritatu na kuvuna magunia 10, sababu kubwa ni nafasi zinazopotea kwenye miraba ya matuta, alisema.

“Ni lazima tuondokane na kilimo hiki kwa sababu hakina tija na tena kinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo lingetumika kupanda mazao,” alisisitiza.

Leo (Jumatatu, Desemba 17, 2012) Waziri Mkuu atakwenda kata za Machimboni na Nsimbo ambako atahutubia wananchi
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger