Pages

Home » » JESHI LA POLISI MBEYA LAINGIA DOSARI KATIKA UWAJIBIKAJI WAKE BAADA YA ASKARI 7 KUTUHUMIWA KUMPIGA NA KUMUOMBA RUSHWA MWANANCHI ALIYEFIKA KITUO CHA POLISI KUTOA TAARIFA DHIDI YA MTUHUMIWA

JESHI LA POLISI MBEYA LAINGIA DOSARI KATIKA UWAJIBIKAJI WAKE BAADA YA ASKARI 7 KUTUHUMIWA KUMPIGA NA KUMUOMBA RUSHWA MWANANCHI ALIYEFIKA KITUO CHA POLISI KUTOA TAARIFA DHIDI YA MTUHUMIWA

 Hapa Mr.LAITONI MWAKALINGA akionesha mkoano wake wa kulia nje ya ofisi za haki za binadamu wilayani Mbozi.(Picha na Mpiga picha wetu)

 Na Mwandishi wetu.Mbozi.
Askari polisi saba wa kituo cha polisi Mbozi wanatuhumiwa kwa kumpiga, kumjeruhi na kumsababishia maumivu makali LAITON MWAKALINGA mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Kijiji cha Haterere.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LAITON MWAKALINGA alipigwa na askari wakati akipeleleka malalamiko dhidi ya shemeji yake aliyemtishia kumuua ambapo askari hao walimtaka atoe kiasi cha shilingi elfu arobaini na alipgoma ndipo walipoanza kumpiga hadi kumvunja mkono.

Kutokana na kitendo hicho Kamanda wa polisi mkoani hapa DIWANI ATHUMANI ameahidi kulifuatilia tukio na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa haraka na sahihi ili hatua za haraka za haraka ziweze kuchukuliwa.

Aidha Kamanda DIWANI amefanya juhudi za kukutana na LAITON MWAKALINGA ofisini kwake na moja ya ahadi aliyoitoa kwa Laiton ni kuhakikisha anapata matibabu ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku. 

Wakati huohuo amesema ni kosa kwa askari yeyote kumpiga raia hata kama amefanya kosa, na kwamba kutokana na kitendo walichofanya askari hao gwaride maalumu la utambuzi lilifanywa wilayani Mbozi na kuwabaini askari 7 kati ya 10 walibainika kuhusika na kitendo cha kumshambulia na kumuomba Rushwa ili waweze kwenda kumkamata mhalifu.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger