Pages

Home » » JIMBO LA SPIKA WA BUNGE LINATIA AIBU, MAKINDA ANGALIA UWEZEKANO WA KUMALIZA CHANGAMOTO YA BARABARA JIMBONI KWAKO

JIMBO LA SPIKA WA BUNGE LINATIA AIBU, MAKINDA ANGALIA UWEZEKANO WA KUMALIZA CHANGAMOTO YA BARABARA JIMBONI KWAKO

 Barabara  za  jimboni kwa  spika Makinda kama  zinavyoonekana
 Magari  yakipita kwa  shida katika barabara  za jimboni kwa Makinda barabara ya Njombe -Ludewa maeneo ya Uwemba
 Spika Makinda siku alipoapa  kuwatumikia  wananchi  wa  jimbo la Njombe kusini

Na Francis Godwin,Njombe
UBOVU huu wa  barabara ya Njombe - Ludewa katika jimbo la Njombe kusini mkoa mpya wa Njombe jimbo linaloongozwa  na   spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Anne Makinda ni usaliti mkubwa kwa wapiga kura .

Nalazimika kusema kutumia kauli ya usaliti kutokana na kipindi kirefu cha miaka 40 ya ubunge wa Mheshimiwa Makinda katika jimbo hilo na hali halisi ya uchakavu wa miundo mbinu katika jimbo lake hilo.

Mbali ya kuwa spika hawezi kutumia nafasi yake kuuliza swali bungeni  juu ya ubovu huo wa barabara ila anayonafasi ya kutumia njia mbadala ya kufikisha kilio cha wananchi wa jimbo hilo juu ya ubovu huo wa miundo mbinu .

Kwani mtazamo wa wageni wanaoingia na kutoka katika jimbo hilo na wapiga kura wa jimbo hilo ni ule wa kufikiri kuwa mbunge wao Makinda amelitelekeza jimbo hilo kwa kujitoa kuwa mwalilishi wao bungeni .

Kwa wenyeji wa jimbo hilo la Njombe kusini na wale wa jimbo la Ludewa wanaweza kuwa mashahidi wazuri wa kero hii ya miundo mbinu katika jimbo la Njombe kusini na iliyopo jimbo la Ludewa.

Hakuna asiyetambua kuwa ukitoka njiapanda ya Songea kuingia barabara ya mvumbi kijiji cha Nundu hadi Luponde barabara yake ni chafu kupita kiasi na ndicho Kipande ambacho wasafiri hukwama na hata vyombo vya usafiri huharibika kutokana na Kipande hicho ambacho kwa madereva hutumia zaidi ya saa moja kupita eneo hilo huku baadhi ya magari hulazimika kulala eneo hilo kusubiri huruma ya mwenyezi Mungu ya kuleta jua ili kuweza kupita vinginevyo kupita hapo ni sawa na ndoto za alinacha .

Hivyo kutokana na ubovu wa Kipande hicho cha Nundu - Luponde katika jimbo hilo la Njombe kusini na uzuri wa miundo mbinu ya Kuanzia mpakani mwa jimbo la Niombe na Ludewa ni wazi waweza kuungana nani kuwa Spika Makinda ameamua kuwasaliti wapiga kura wake na kutumia miaka 40 ya ubunge wake kwa kuwaacha wapiga kura katika maswali mengi zaidi kuliko majibu .

Hivi ni nani asiyetambua kuwa wapiga kura wa jimbo la Njombe kusini ni miongoni mwa wapiga kura wenye bahati kubwa kwa mbunge wao kuendelea kuwa chaguo la Taifa kwa kushika nafasi kubwa za kitaifa ikiwa ni pamoja na kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uongozi wa spika Samweli Sitta na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wananchi wa jimbo hilo waliweza kujenga Imani kubwa ya kumchagua tena na wabunge kujenga matumaini makubwa na kumchagua kuwa spika wa kwanza Mwanamke na kuweka historia ndani ya nchi na barani  Afrika Kama si duniani.

Sipendi kwa leo kuhusiana utendaji wake Kama spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na uwakilishi wake kama mbunge wa jimbo la Njombe kusini ,japo hakuna asiyetambua kuwa Kati ya ma spika walioonyesha kupwaya kukikalia kiti hicho cha uspika na Kama utatakiwa kuwataja kwa majina basi ni vigumu kuliacha kulitaja jina la Mheshimiwa Anne Simamba Makinda mbunge wa jimbo la Njombe kusini.

Pamoja na kuwa mapungufu ni kawaida kwa kiongozi awaye yeyote yule ila yapo mapungufu mengine ambayo ni aibu kwa kiongozi moja ya mambo yanayoweza kumpa kiongozi aibu na kuchokwa zaidi na wale anaowaongoza kwa kero Kama hizi za miundo mbinu Kwani unapozungumzia maendeleo ya jimbo na wananchi ni vigumu kuacha kuangalia usalama wa miundo mbinu ,Elimu ,chakula  ,afya ya wale unaowaongoza .

Hivyo Kama kiongozi mwakilishi wa wananchi umeshindwa kuwatetea ama kusimamia ujenzi wa miundo mbinu bora na kuacha eneo Lake analoliongoza bila  kuwa na miundo mbinu mizuri  ni wazi hakuta kuwa na maendeleo na usalama wa chakula ,afya na Elimu utaendelea kuwa mashakani zaidi.

Kwa upande wa jimbo la Njombe na wilaya nzima ya Njombe ni moja Kati ya maeneo ambayo wananchi wake wanategemea zaidi kilimo hivyo kuendelea kuiacha miundo mbinu ambayo ni barabara bila kutegeneza ni wazi ni kuwakomoa wananchi hao ambao wanategemea miundo mbinu kamili ili kujikwamua katika dimbwi la umasikini.

Ikumbukwe kuwa hii ni miaka 50 sasa toka nchi yetu ilivyopata Uhuru wake mwaka 1961 hivyo ilipaswa kuwa ni matumaini Mapya Kwa waanchi wa pembezoni mwa Tanzania kuona miundo mbinu bora inakuwepo katika maeneo Yao na hata ikiwasaidia kuona jitihada za ujenzi wa barabara za lami katika maeneo Yao.

Leo ni aibu kwa Taifa kuona wilaya  Kama Njombe,Ludewa na Mufindi hazi barabara za lami wakati katika maeneo hayo yamekuwa yakiongoza kusaidia uchumi wa Taifa kukua zaidi.


Wakizungumzia hali hiyo ya ubovu wa barabara katika barabara jimbo la spika Makinda  wananchi wa kijiji cha Nundu na  Luponde walisema  kuwa eneo hilo la Nundu na Luponde ambalo limekuwa likisumbua  zaidi kipindi cha masika  na hata kupelekea  mabasi ya abiria kukwama lina urefu wa takribani   Kilometa 63  ambazo mabasi hutumia muda wa zaidi ya masaa matatu badala ya dakika 30 hadi 45  Kama ilivyo lami

Yohana Sanga ambaye ni mkazi wa kijiji cha Luponde alisema kuwa ubovu wa barabara hiyo iliyopo jimboni kwa spika wa bunge imekuwa ni kero kubwa na hata kupelekwa wananchi kuendelea kujenga chuki na serikali ya CCM na mbunge huyo kwa kushindwa kuimaliza kero hiyo.

Sanga alisema kuwa  kutokana na kero hiyo ya ubovu wa barabara wapinzani wameendelea kuliteka jimbo hilo la Njombe kusini na kuweka ngome yao kwa madai kuwa mbunge wao spika Makinda amelitelekeza jimbo hilo .

Kwani alisema kuwa haiwezekani jimbo hilo kuendelea kuwa na barabara mbovu Kama hiyo wakati Mbunge wao ni mmoja Kati ya viongozi wakubwa nchini na walitegemea nafasi yake katika Taifa kuwa ni sehemu ya ufumbuzi wa kero za miundo mbinu inayowakabili wananchi wa jimbo la Njombe kusini.

Makinda amekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa akitokea Njombe na amekuwa mbunge kamili wa jimbo toka mwaka 1995 hadi sasa na amepata kushika nafasi ya unaibu spika na uspika kamili mwaka 2010 ila bado ameshindwa kutumia vema nafasi yake Kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Njombe kusini wala kutumia heshima ya uspika kuelekeza maendeleo jimboni kwake.

Katakana na uwajibikaji mbovu  wa Makinda kwa wapiga  kura wake imekuwa ni mwanzo wa jimbo la Njombe kusini kuwa ngome ya Vyama vya upinzani hasa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambacho kimefanikiwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama na mashabiki katika jimbo hilo huku bendera za CCM zikishushwa na kuwekwa za Chadema.

Japo sina uhakika kuwa wote wameamua kuhama CCM katakana na uwajibikaji mbovu wa mbunge wao ila Kama wahenge walivyonena kuwa dalili za mvua ni mawingu basi tuchukulie haya ni mawingu Makinda na CCM yake wajiandaa kwa miamvuli ili kujihamia na mvua Kali .

Dalili za mbunge kushindwa katika uwakilishi wake kwa wananchi zipo Nyingi moja ni utendaji na kauli zake na pili mtazamo wake na wananchi dhidi yake ambapo mtazamo wa Makinda mwenyewe kwa wapiga kura wake ni huu wa kuwachukulia wapiga kura Kama ni watu wanaotegemea kuomba Pesa Kutoka kwake hadi kufikia hatua ya kuwakimbia na kuwalalamikia katika vikao vya Chama kuwa wapiga kura omba omba ambao kila wakimwona wanataka Pesa.

Sitaki kumwagiza spika wangu Makinda kuwaomba radhi wapiga kura wake kwa kuwaita omba omba ila namwangukia na kumlamba miguu kumwomba kutorudia tena kauli Kama hiyoaliyoitoa katika kikao cha kwanza cha Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi( CCM) kilichohudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wabunge wote wa mkoa wa Njombe Kama Deo Filikunjombe, Dr Binilith Mahenge, Deo Sanga, Gyerson Lwenge ,Pindi Chana na Lediana Mng,ong,o na makanda wa CCM.

Hivi hebu tujiulize Leo Makinda ambae ameongoza jimbo hilo toka mwaka 1995 hadi sasa Kama Vipindi vinne sasa ameshindwaje kufanya japo kitu kimoja cha kuonekana na kusingizia Pesa hakuna wakati jirani yake mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kwa Kipindi chake cha kwanza tu ameanza kuonyesha mafanikio Makubwa Ludewa hata kuweka historia ya Karne kwa kuanza ujenzi wa lami Ludewa ambayo haijapata kuwepo toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961? Ni vema CCM kuacha kuwachukia wanachama wanaofanya vema na kusema ukweli kuwa nimaadui na kuendelea kuwakumbatia wabunge Kama Makinda kuwa ni wema huku wapiga kura wakiwaona Kama ni maadui hivyo ili nchi iweze kusonga mbele katika maendeleo ni lazima wabunge Kama akina Makinda tukawapumzisha pembeni na kuweka wabunge watendaji .
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger