MWANZA, TANZANIA
Baada
ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA wilayani Ilemela, kuupiga ‘stop’ uongozi
wake wa wilaya, sasa unatishia kuwang’oa madiwani wake saba, wanaodaiwa
kushindwa kulinda kiti cha Meya wa jiji la Mwanza.
Madiwani
hao wanadaiwa kukisariti chama hicho kwa kuongoza harakati za kumng’o
aliyekuwa Meya wa jiji hilo , Jacton Manyerere, mwezi uliopita baada ya
kuungana na madiwani wa vyama vingine kumpigia kura za kutokuwa na imani
naye.
Habari
zilizopatikana hapa kutoka ndani ya Chadema zimetonya kuwa, Mkutano
Mkuu wa wilaya ya Ilemela, uliofanyika Agosti 12 mwaka huu katika hoteli
ya PK wilayani humo, ‘uliwaka moto’ baada ya kuibua hoja ya kutokuwa na
imani na viongozi wa mkoa pia madiwani hao.
Kwa
mujibu wa habari hizo, wajumbe na viongozi wapya wa wilaya hiyo
watatoana macho na uongozi wa mkoa ambao unadaiwa kutafuna fedha za
ruzuku zilizotolewa mkoani Mwanza.
Imedaiwa
kwamba, moja ya mambo yaliyohojiwa katika mkutano huo na kusababisha
uwake ‘moto’ ni pamoja na ruzuku hiyo, ambayo Katibu wa Chadema mkoani
Mwanza, Wilson Mushumbusi ameshindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi
yake katika vikao husika.
“Hadi
kieleweke vinginevyo tutatona macho kama mapato na matumizi ya ruzuku
hayataeleweka.” Kilisema chanzo kimoja kutoka ndani ya uongozi wa wilaya
hiyo na kudai kuwa wajumbe wengi wa kikao hicho wanataka Madiwani hao
wakiwemo wawili wa Viti Maalum, walioshindwa kulinda kiti cha Meya wa
jiji hilo , wang'olewe.
“Waliungana
na madiwani wa CCM na CUF kumpigia kura za kutokuwa na imani naye
mheshimiwa Manyerere aliyekuwa Meya wetu, ni wasaliti hawafai,
wamekiangusha chama, wanapaswa kuwajibishwa kama ulivyong’olewa uongozi
wa wilaya hii.” Kilifafanua chanzo hicho.
Madiwani
hao walitajwa kuwa ni Abukari Kapera(Nyamanoro), Hamis Kijuu (Mbugani),
Adamu Chagulani (Igoma), Henry Matata (Kitangiri), Marietta Chenyenge
(Ilemela), Lucy Kazungu na Upendo Robert, wote viti maalum.
0 comments:
Post a Comment