Na Sammy Jumaa Kisika, Rukwa.
Mahakama
ya hakimu mkazi wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, imemhukumu mkazi wa
kijiji cha Katazi wilayani humo Geradi Choma (37) ,adhabu ya kifungo cha
maisha jela kwa kosa la kumbaka mwanae wa kambo mwenye umri wa miaka
tisa.
Adhabu
hiyo imetolewa na hakimu wa mahakama hiyo Mh. Adamu Mwanjokolo, baada
ya Geradi kukiri mahakamani hapo kuwa alitenda kosa hilo Julai 7 mwaka
huu majira ya saa sita usiku wakati mkewe akiwa safarini mjini
Sumbawanga.
Mwendesha
mashtaka toka jeshi la polisi Mkaguzi Msaidizi Emmanuel Shani katika
ushahidi wake, amesema kuwa siku hiyo usiku baada ya Geradi kurejea
kutoka kwenye matembezi yake alimkuta binti huyo akiwa amelala chumbani
na watoto wenzake, lakini alimwamsha na kumpeleka kwenye chumba cha
wazazi wake kisha kumbaka na kumtishia kuwa atamroga iwapo
angelimwambia mtu yeyote kuhusiana na kitendo alichofanyiwa.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Mwanjokolo amesema kitendo alichofanya Geradi ni cha
hatari na aibu hivyo anastahili adhabu hiyo, ili iwe fundisho kwa watu
wengine wenye kufanya vitendo kama hivyo.
0 comments:
Post a Comment