Mfanyakazi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Iringa (IRUWASA) akiwajibika kuzibua chemba iliyozibwa na kulalamikiwa na wananchi kupitia mtandao huu wa radio Nuru Fm asubuhi ya leo
Diwani wa kata ya Makorongoni Iringa na wananchi wakishuhudia zoezi la kuzibua chemba iliyoziba
Baada ya wananchi kuulalamikia ungozi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Iringa (IRUWASA) kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa kuzibua chemba zilizozibwa ,wafanyakazi hao wamefika eneo la tukio asubuhi hii kuzibua chemba hiyo iliyolalamikiwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa
BAADA YA HALI HIYO DIWANI ATOA MWEZI MMOJA KWA WANANCHI WAKE KUACHA MARA MOJA KUTUPA TAKA OVYO.
Hali ya uchafu katika eneo la mwembetogwa ambapo wananchi wanatupa taka katika mto mchambawima baada ya kukosa chombo cha kuwekea taka
Chemba za maji taka kutoka katika vyoo zikiwa zimefumka bila matengenezo kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Iringa (IRUWASA)
Diwani Tenga akitoa muda wa mwezi mmoja kwa wananchi wake kuacha kutiririsha maji ovyo
Diwani wa kata ya Makorongoni mjini Iringa Mhe.Tadeus Tenga ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wananchi wa kata hiyo kuacha kutiririsha maji taka ovyo huku akiitaka mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Iringa (IRUWASA) kufanya kazi bila kusukumwa na wananchi .
Diwani Tenga ametoa kauli hiyo leo katika mahojiano maalum na Jamii yangu.
Amesema kuwa hali ya usafi katika kata hiyo ni mbaya sana na kuwa kutokana na hali hiyo amelazimika kutoa muda wa mwezi mmoja kwa wananchi wa kata hiyo kufanya usafi huku akiijia juu Iruwasa kwa kutaka kutembelea maeneo mbali mbali badala ya kukaa ofisini.
Diwani huyo amekili kuwa hali ya ufisa na chemba za maji taka kuziba katika eneo hilo kuwa ni sugu na hivyo kutaka jitihada za haraka kufanyika ili kuepusha kipindu pindu
0 comments:
Post a Comment