Pages

Home » » Mgogoro Wa Ardhi Kapunga Wilayani Mbarali – 2

Mgogoro Wa Ardhi Kapunga Wilayani Mbarali – 2

Ujio wa Nafco na maombi ya ardhi HUU ni mfululizo wa Ripoti Maalum kuhusiana na mgogoro wa ardhi Kapunga wilayani Mbarali, mkoani Mbeya kama unavyoendelea kusimuliwa na Mwandishi Wetu DANIEL MBEGA, ambaye aliyefanya uchunguzi kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu kwa ufadhili mkubwa wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) kupitia Mpango wa Mafunzo Maalum (Fellowship). Endelea na Sehemu hii ya Pili…

KAULI mbiu za Siasa ni Kilimo; Ukulima wa Kisasa; Kilimo cha Kufa na Kupona; Chakula ni Uhai; na sasa Kilimo Kwanza, zote zimekuwa na madhumuni ya kuendeleza kilimo ambacho kinatajwa kwamba ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.
Serikali ya Tanzania baada ya uhuru ilitambua umuhimu wa kukiendeleza kilimo, ambacho hata hivyo kilikuwa na changamoto nyingi kutokana na kutegemea zaidi mvua za masika na vuli, ambapo zilipokosekana hali ilikuwa mbaya sana kama ilivyotokea katika ukame wa mwaka 1966.
Hali hiyo ndiyo iliyoifanya Serikali ya Tanu wakati huo kuja na kauli mbiu mbalimbali ili kukipa kipaumbele kilimo kwa kutambua kwamba asilimia 83 ya Watanzania wanakitegemea kwa uchumi pamoja na kuchangia pato la Taifa.
Katika kutimiza malengo ya mkakati wa maendeleo kupitia utaratibu wa kujitosheleza kwa chakula Serikali ya Tanzania iliamua kupanua kilimo cha umwagiliaji kuimarisha juhudi za uzalishaji za wakulima wadogo katika maeneo yaliyotegemea mvua pekee.
Mwaka 1969 Shirika la Taifa la Kilimo na Chakula (Nafco) likaanzishwa rasmi likiwa na jukumu la kutekeleza na kusimamia miradi ya kilimo cha mazao yote, ukiondoa miwa. Nafco ikawa na majukumu ya kusimamia mazao ya chakula kama mahindi, mpunga na maharage, na mazao ya biashara kama kakao na minazi huku pia ikihusika na usafirishaji na uhifadhi wa mazao hayo.
Hadi kufikia katikati ya miaka ya 1970 shirika hilo lilikuwa limefanya kazi nzuri kulinganisha na mashirika mengine yaliyoanzishwa na Serikali kwa majukumu ya kusimamia shughuli nyingine za uchumi katika sekta ya umma. Tayari lilikuwa limeanzisha mashamba makubwa ya umwagiliaji huko Mbarali na Ruvu. Katika program yake ya maendeleo ya mpunga, Nafco iliamua kutumia umwagiliaji kama njia ya kukabiliana na ukame, hivyo kuwa na kilimo cha uhakika
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger