Pages

Home » » UVCCM UCHAGUZI LEO

UVCCM UCHAGUZI LEO



WAKATI Uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umemalizika juzi, huku ukidaiwa kugubikwa na ubabe na rushwa, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umejitapa kwamba, utahakikisha vitendo hivyo havitokei katika uchaguzi wake mkuu utakaofanyika kuanzia leo mjini Dodoma.
UVCCM imeapa kwamba mgombea au hata mpambe atakayebainika kujihusisha na kampeni zilizo nje ya utaratibu na kanuni za UVCCM au kujihusisha na vitendo vya rushwa atashughulikiwa mara moja ikiwemo kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM,Martine Shigela alisema, wameweka mtandao mpana wa kutosha kukabiliana na aina yoyote ya ukiukwaji wa tararibu, kanuni na sheria za uchaguzi wa UVCCM.
Shigela alisema, taratibu za mkutano mkuu utakaoambatana na uchaguzi huo, zimekamilika na utafanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, uliopo Chuo Cha Mipango ambako ndiko ulikofanyika pia ule wa UWT.
Amesema, mkutano unaanza leo, Oktoba 23, na utafunguliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wanachuana wagombea watatu, Lulu Mushamu Abdallah,  Sadifu Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka wakati katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ally Salum Hapi, Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita.
Nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti vitano Zanzibar wagombea 14,  Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger