Pages

Home » » SERIKALI YATISHIA KUWATIMUA WAWEKEZAJI WA TANZANITE ONE

SERIKALI YATISHIA KUWATIMUA WAWEKEZAJI WA TANZANITE ONE



Serikali imetishia kuwatimua wawekezaji wa kampuni ya madini ya Tanzanite one iliyopo Mererani wilayani Simanjiro iwapo watashindwa kulipa deni la zaidi ya dola za kimarekani milioni 2.2 zilizotokana na ukwepaji kodi .
Katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi ametangaza msimamo wa serikali wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini baada ya kugundulika kuwa yapo makampuni kadhaa yamekuwa yakiendesha shughuli zake za madini bila kulipa ushuru wa serikali kinyume cha sheria.
Akizungumza na chama cha wanunuzi na wauzaji wa madini nchini TAMIDA,jijini Arusha jana,Maswi alisema kuwa kampuni ya Tanzanite one imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya mrahaba wa madini tangu mwaka 2004 hadi 2008 na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 3.4 fedha za kitanzania.
Amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikitumia ujanja wa kukwepa kulipa mrabaha wa  mauzo pale inapokuta soko la madini nje ya nchi limeongezeka na kwamba serikali kupitia kitengo cha ukaguzi wa madini iliweza kubaini ukwepaji huo wa kodi na kuiamuru kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha au ifungashe virago.
Ameongeza kuwa iwapo kampuni hiyo ingegoma kulipa deni hilo serikali ilikuwa tayari kuwatimua na kuwamilikisha wazawa mgodi huo.
Kwa mujibu wa kamishina wa madini kanda ya kaskazini Benjamin Mchwampaka alisema kuwa tayari kampuni hiyo imeshaanza kulipa deni hilo na kwamba hadi sasa  imeshatoa malipo ya dola 200,000 zaidi ya fedha za kitanzania milioni 310,huku serikali ikiitaka kuhakikisha inamaliza kulipa deni hilo hadi kufikia jamuari mwaka 2013.
Hata hivyo katibu huyo ameitaka TAMIDA kuisaidia serikali kuyafichua  makampuni yanayokwepa kulipa ushuru wa madini wakiwemo baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ili wachukuliwe hatua na kusisitiza kuwa kwa sasa serikali imeanza mkakati wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger