Diwani wa kata ya Ruhuhu Edwin Haule Spika
Katika hali isiyotegemewa mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe alilazimika kumnusuru diwani wa kata ya Ruhuhu Bw Edwin Haule Spika kuzomewa na wapiga kura wake baada ya kudaiwa kushindwa kutimiza ahadi yake ya shilingi 50,000 ambayo aliitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010.
Wakizungumza katika mkutano huo kwa jazba mbele ya mbunge huyo wananchi wa kata ya Ruhuhu walisema kuwa hawana imani hata kidogo na diwani wao huyo mheshimiwa Spika kutokana na kuwatapeli kiasi cha shilingi 50,000 ambacho aliahidi wakati wa kampeni na hivyo kudai kuwa hawapo tayari kumsikiliza katika mkutano huo wa mbunge ambao ni kwamara ya kwanza wanamwona diwani huyo toka uchaguzi mkuu wa mwaka2010.
Grece Haule alisema kuwa diwani huyo aliahidi fedha hizo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Zahanati ulioanza toka mwaka 2004 hadi sasa bila kukamilika na kuwa mbali ya kuwa Halmashauri ni kikwazo cha kukamilika kwa Zanahati hiyo ila diwani wao pia anachangia kwa kiasi kurudisha nyuma maendeleo .
Kutokana na madai hayo ya wananchi mbunge Filikunjombe alilazimika kumsimamisha diwani huyo ili kutekeleza ahadi hiyo ila hakuweza kuanya hivyo kutokana na kukosa kiasi hicho cha fedha na hivyo kuwaomba wapiga kura wake kuendelea kumvumilia mkopo huo wa ahadi hadi hapo atakapofanikiwa kupata fedha.
" Mheshimiwa mbunge na wananchi naomba kupewa muda nitakaa na wananchi ili kumaliza deni hilo ....naomba mnivumilie "
Kutokana na diwani huyo kushindwa kulipa fedha hizo mbunge alilazimika kumlipia fedha hizo kiasi cha shilingi 50,000 na kuwaongeza kiasi cha shilingi 500,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa wodi la mama na mtoto kijijini hapo.
0 comments:
Post a Comment