Pages

Home » » Dk. Mukangara alipowatembelea vijana na saccos zilizonufaika na fedha za mkopo wa mfuko wa vijana mkoa wa Mwanza

Dk. Mukangara alipowatembelea vijana na saccos zilizonufaika na fedha za mkopo wa mfuko wa vijana mkoa wa Mwanza

 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  akiongea jambo na Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Maendeleo Vijana  James Kajugusi  (aliyevaa suti ya blue) jana mara baada ya kumaliza kuwatembelea vijana wajasiriamali wa soko kuu la jijini Mwanza ambao  walipata mkopo kutoka mfuko wa vijana kupitia  Halmashauri ya jiji. Waziri Dk. Mukangara aliwatembelea wajasiliamali hao ili  kuona fedha walizopata zimewasaidiaje  kama kundi la vijana na kijana mmojammoja.
Mwenyekiti wa SACCOS ya Wafanyabiashara Wadogowadogo Mkoa wa Mwanza (WADOKI)  Mussa Ally akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia) mfano wa jengo wanalolitarajia kujenga hivi karibuni kama kitega uchumi chao jana jijini Mwanza. SACCOS hiyo ilipata mkopo kutoka mfuko wa vijana mwaka 2009 fedha ambazo waliwakopesha vijana wanachama 12.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (katikati) akimsikiliza Jummanne Izengo (kulia) ambaye alimueleza jinsi alivyonufaika na mkopo alioupata kutoka mfuko wa vijana ambao umemuwezesha   kununua mashine ya kusaga nafaka,  kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Vijana  James Kajugusi . Waziri Dk. Mukangara alimtembelea Izengo jana katika eneo lake la biashara lililopo Mwaloni jijini Mwanza ili kuona fedha alizopata zimemsaidiaje  kama kijana.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akiongea jambo na  Songaleli Mzee (kulia) ambaye ni mfanyabiashara wa soko kuu la jijini Mwanza aliyepata mkopo kutoka mfuko wa vijana na kufanya biashara ya nafaka. Katikati ni Edward Kabululu  ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza SACCOS ambayo ni moja kati ya 14 za mkoa wa Mwanza zilipata fedha za vijana mwaka 2009 na kumpatia mkopo  Mzee.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (katikati) akiongea na wafanyakazi wa SACCOS ya Wafanyabiashara Wadogowadogo Mkoa wa Mwanza (WADOKI) jana jijini Mwanza juu ya umuhimu wa kuwahimiza wanachama wao hasa vijana kuitumia mikopo wanayoipata katika shughuli  za kilimo cha chakula, ufugaji wa samaki na uvuvi ili kuisaidia nchi kuepukana na tatizo la njaa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi na kushoto ni Mwenyekiti WADOKI SACCOS  Mussa Ally.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akimuangalia mteja akisukwa nywele katika Saluni ya Juvee Kanuzile  (hayupo pichani) ambaye alipata mkopo kutoka mfuko wa vijana kupitia halmashauri ya jiji mwaka 2009 na kufanya biashara ya saluni. Waziri Dk. Mukangara alitembelea saluni hiyo ili kuona fedha alizopata Kanuzile zimemsaidiaje  kama kijana.
  Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger