Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na waumini wa
kanisa la Anglikanala watakatifu wote Jimbo la Ziwa Rukwa mjini
Sumbawanga jana katika ukumbi wa RDC mjini Sumbawanga katika jitihada
zake za kuunganisha dayosisi hiyo baada ya kuwa na mpasuko wa muda mrefu
wa zaidi ya miaka miwili wa makundi mawili moja likiwa linatii mamlaka
ya kanisa Anglikan kwa kumkubali Askofu Kasagara kama kiongozi wao
kanisani aliyesimikwa mwaka jana tarehe 16, Juni kwa mujibu wa katiba ya
kanisa hilo na wengine wanaompinga kwa madai kuwa hana sifa za kuwa
kiongozi wao na kwamba kwenye uchaguzi uliomchagua alitumia rushwa.
Katika
kikao kilichodumu kwa zaidi ya masaa nane ikiwa ni dhamira ya Mkuu huyo
wa Mkoa kutafuta suluhu ya migogoro yote iliyopo Mkoani Rukwa ukiwepo
huu wa kanisa Anglikan muafaka ulishindwa kupatikana kutokana na upande
unaompinga askofu kuchelea kutoa maamuzi ya kuteua wajumbe watano
watakaoungana na wajumbe wengine watano kutoka upande wa wanaotii
mamlaka kushirikiana na Kiongozi huyo wa Mkoa kutafuta suluhu ya mwisho
kushindikana na kudai wapewe muda zaidi kutafakari yote yaliyozungumzwa
na ndipo wafanye uteuzi wa wajumbe hao.
Baada
ya ushawishi mkubwa uliotumika Mkuu wa Mkuu wa Rukwa aliona kuwa
dhamira halisi ya kumaliza mgogoro huo kwa baadhi ya waumini hususani
wanaompinga Askofu haipo na kwamba msimamo wao uko pale pale wa kumpinga
kiongozi huyo. Alihitimisha kwa kusema kuwa ataandika taarifa yake na
kuifikisha panapostahiki taarifa itakayoonyesha kuwa kundi moja lipo
tayari kutoa ushirikiano wa kumaliza mgogoro na lingine linalompinga
Askofu Kasagara kutokuwa na utayari wa kutoa ushirikiano unaostahiki.
Alimalizia kwa kusema kuwa ataliandikia Kanisa lichukue maamuzi
kulingana na taratibu zao za kikanisa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na waumini wa
Kanisa hilo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RDC) jana.
Baadhi ya waumini wa kanisa
la Anglikana watakatifu wote Jimbo la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga
wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo wa Mkoa aliyekuwa akijaribu kuwaweka
sawa juu ya umuhimu wa kuungana na kuacha tofauti zao kwa maendeleo ya
kanisa lao na Mkoa kwa ujumla. Baadhi ya waumini hususan wanaompinga
Askofu wa kanisa hilo jimbo la Ziwa Rukwa wameweka msimamo wao kuwa
hawamtaki kiongozi huyo
0 comments:
Post a Comment