WIZARA
ya Afya na Ustawi wa Jamii inatarajia mwaka ujao kuanzisha chanjo mpya
mbili za Pneumococcal na Rotavirus, ambazo ni maalum katika kukinga
maradhi na vifo kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.
Kauli hiyo
ilitolewa jijini Dar es Salaam leo, na Mkurugenzi wa Kinga, Elias
Chinamo, wakati wa warsha ya siku moja ya wandishi wa habari, ya
kuwajengea uwezo wa kufilisha elimu sahii kwa jamii pamoja na kuihamasisha jamii kuhusu chanjo hizo mpya, zitakapoanza mwaka 2013.
Alisema walengwa wa chanjo hizo
watakuwa ni watoto waliyonaumri wa chini ya miezi 12 ambapo chanjo ya
kukinga nimonia (pcv13), itatolewa mara tatu kuanzia umri wa wiku sita,
10 na 14.
Chinamo akubainasha kuwa chanjo
ya kinga ya kihara (rotavirus), itatolewa mara mbili kuanzia imri wa
wiku sita na 10, inasisitizwa kuwa ili mtoto apate kinga lamili ni
lazima akamilishiweratiba mapema.
Alisema kitaalam zinaonesha kuwa
chanjo ya ‘Pneumococcal’ hukinga maambukizi ya nimonia kwa asilimia 38,
homa ya uti wa mgongo kwa takriban asilimia 87; na chanjo ya
‘rotavirus’ hukinga kuharisha kuharisha kunakosababisha vifo vya watoto
kwa aslimia 80.
0 comments:
Post a Comment