Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wajumbe wa
semina elekezi ya madiwani wa CCM wa Mkoa wa Rukwa wakati akifunga
semina hiyo iliyoanza jana na kumalizika leo katika ukumbi wa Manispaa
ya Sumbawanga. Kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa Ndugu
Hiporatus Matete. Semina hiyo iliyokuwa ya mafunzo ilikuwa na lengo la
kuimarisha utendaji kazi wa chama hicho pamoja na kukiongezea chama
uwezo zaidi wa kuisimamia shughuli za Serikali katika utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi wa chama hicho pamoja kukiongezea nguvu zaidi kiweze
kushinda katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015.
Semina
hiyo ilikuwa na jumla ya mada tisa amabazo ni historia ya CCM tangu
TANU na ASP, Katiba ya CCM ya mwaka 1977-2012, Sera za msingi
za CCM, Muelekeo wa Sera za CCM mwaka 2010-2020, Sera za Umma,
Utekelezaji wa sera Ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea katika mazingira ya
utandawazi na uchumi wa soko, Hali ya kisiasa na mikakati wa ushindi kwa
ajili ya uchaguzi Mkuu 2015, Uandishi wa katiba mpya ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania na Majukumu yatokanayo na taarifa ya kazi na
maazimio ya Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM 2012.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete, Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Muwezeshaji wa Semina hiyo
kutoka Sekretarieti ya CCM na Mbunge wa Jimbo la Kalambo CCM Ndugu
Josephat Kandege ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Semina hiyo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete akizungumza
kwenye ufunguzi wa semina hiyo jana. Katika maneno yake ya ufunguzi
alisema lengo kuu la semina hiyo ni kuimarisha chama kiweze kushika dola
kwa kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Rukwa na taifa kwa
ujumla. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisema Serikali haiwezi
kufanya kazi peke yake bila ya msukumo kutoka katika chama, aliwataka
viongozi katika ngazi zote kuwa mstari wa mbele katika kufanya shughuli
za maendeleo badala kukaa tu ofisini na kuagiza walio chini yao.
Kiongozi wa wakufunzi wa semina hiyo Ndugu Lukasi Kisasi akijitambulisha kwa wajumbe wa semina hiyo.
Baadhi
ya madiwani waliohudhuria semina hiyo wakiskiliza kwa makini moja ya
mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo, jumla ya madiwani 64
wameshiriki kwenye semina hiyo.
Madiwani kutoka kata tofauti za Mkoani Rukwa wakifuatilia semina hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza katika Semina hiyo. (Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
0 comments:
Post a Comment