Pages

Home » » MTOTO WA MIAKA 2 ABAKWA AUMIZWA

MTOTO WA MIAKA 2 ABAKWA AUMIZWA


Matukio ya ubakaji watoto wadogo yameendelea kujirudia mkoani hapa baada ya mtoto wa (jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka 2 na miez 6 mkazi wa Ilboru kubakwa hadi kulazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru jijini Arusha.
Tukio hilo la kutisha limetokea jana majira ya asubuhi kwenye mtaa huo wa Ilboru kwa kijana wa miaka 20 nae ni mkazi wa mtaa huo kufanya kitende hicho cha kinyama baada ya mama wa motto huyo kutoka na kumuacha mtoto huyo akicheza na wenzake na ndipo mtuhumiwa huyo kujifanyia anavyotaka kwa mtoto huo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hospitali ya mkoa mama wa mtoto huyo aitwae Mariam Miller mwenye umri wa miaka 30 alisema kuwa yeye alipotoka kidogo kumsindikiza jirani yake aliporudi alimkuta mtuhumiwa akiwa anavaa suruali baada ya kumaliza kitendo hicho huku motto wake akilia kwa nguvu hali iliyomshitua na ndipo alipoanza kumuuliza mtuhumiwa lakinmi alianza kukimbia bila ya kutoa majibu.

Alisema kuwa alipo mkagua alimkuta mwanae ana mabaki ya manii kwenye sehemu zake za siri na ndipo alipowaeleza nduguze waliomshauri kumpeleka hospitali kwa matibabu na hivyo walimpeleka hospitalini hapo kwa matibabu zaidi lakini kabla ya kupewa huduma wauguzi hospitalini hapo walimtaka kupeleka PF3 ya polisi na ndipo alitoa taarifa polisi.

Wakati waandishi wapo wakiendelea kumuhoji mama huyo walipata taarifa za mtoto mwengine wa kike mwenye umri wa miaka 10 (jina tunalihifadhi) aliyebakwa na kijana wa miaka 30 wote wakazi wa mtaa wa Pangani kata ya kati jijini hapa na kesi yake ipo polisi kwa uchunguzi.

Akielezea mbele ya waandishi wa habari bibi wa mtoto huyo Zahra Mohamed alisema kuwa yeye anajishughulisha na biashara ya kuuza vitafunwa kwenye stand kuu ya mabasi jijini hapa alipotoka kweda kwenye shughuli zake kuna kijana wa nyumba ya jirani huwa anakuja nyumbani hapo mara kwa mara kama nyumbani lakini hakugundua kama kuna mchezo mchafu unaendelea nyuma wakati akitoka lakini za nmwizi arubaini juzi majira ya jioni alirudi nyumbani ghafla ndipo alimkuta kijana huyo uani kwao na binti alipomwita alichelewa kuja na alipokuja alikuwa na wasiwasi mwingi ndipo mama yake mkubwa alianza kumchapa ili amweleze kwanini analia na kuwa na wasiwasi ndipo alipomba asichapwe ataeleza ukweli
Zamzam alisema kuwa hiyo si mara ya kwanza bali kila mara kijana huyo aliyefahamika kwa jina Moja la Yasin alikuwa akimuingilia na kumpa shilingi mia mbili kama ujira wa kufanya nae kitendo hicho huku akimtisha akisema atampeleka polisi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazazi na walezi hao walisema kuwa wanaiomba serekali mkoani hapa kuyacvhukulia kwa uzito matukio hayo ya ukatili wa kuwabaka watoto wadogo kwani kwa siku za hivi karibuni matukio hayo yamekithiri kwenywe mitaa mbali mbali ya jiji hili
Kamanda wa Polisi Liberatu Sabas alisema kuwa jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na uchunguzi wa matukio hayo na kuwa watuhumiwa wote wakikamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukuwe mkondo wake na kuwataka wakinamama kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kubaini au kukabiliana na vitendo hivyo.
Imeandikwa na Mahmoud Ahmad, Arusha-Tanzania.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger