Pages

Home » » Mwandishi Aliyepigwa Risasi Anaendelea Na Matibabu MOI

Mwandishi Aliyepigwa Risasi Anaendelea Na Matibabu MOI


Ndugu wapendwa, DSM City Press Club imepata taarifa za kushtusha kufuatia ya kupigwa risasi na kujeruhiwa begani kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama wa Dar City Press Club (DCPC). 
 
Sambamba na taarifa hizo imeelezwa kuwa mwandishi huyo amelazwa katika Taasisi ya mifupa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI). 
 
Chanzo hasa cha kupigwa risasi kwa mwandishi huyo bado hakijaeleweka kwa DCPC, uongozi wa DCPC unafuatilia. Tutakapojiridhisha na taarifa zilizotolewa pamoja na zile tutakazozipata tutawataarifu rasmi. Kwa sababu hizo tunaomba waandishi wote, ndugu, jamaa, marafiki, wapenda haki na amani, wanaharakati washirika na wadau wote wa vyombo vya habari kuwa watulivu tukimjulia hali kwa misaada ya hali na mali mwandishi mwenzetu Shabban Matutu ili apone majeraha
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger