Pages

Home » » WAZIRI HAWA GHASIA AFUNGUA MKUTANO WA WABUNGE NA MADIWANI WA DAR ES SALAAM

WAZIRI HAWA GHASIA AFUNGUA MKUTANO WA WABUNGE NA MADIWANI WA DAR ES SALAAM

  
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia ameziagiza Halmashauri na Jiji la Dar es Salam kujadiliana na kupata sheria nakanuni zitakazo ainisha utendaji kazi wao.
Kauli hiyo ilitoa jijini jana, na waziri huyo, wakati akifungua mkutano wa wabunge na madiwani, wa mkoa huo, kwa ajili ya majadiliano, kuhusu mustakabali wa jiji hilo.
 
Ghasia alisema kutokana na mkanganyiko wa kazi za Mamlaka ya Jiji na zile za Halmashauri kutoeleweka, mnapaswa kujadiliana hususan kuboresha sheria na kanuni zake ili kuimarisha mahusiano, kupata sheria na kanuni zitakazo tambulisha mipaka ya mamlaka hizo mbili kiutendaji.
Akizungumzia mradi wa Mabasi ya endayo haraka (DART), alisema lengo la mradi huo, ni kuwa na usafiri bora wa Umma wenye gharama nafuu, unaotumia mabasi makubwa.
Ghasia alisema dhima ya Mradi huo ni kutoa huduma bora na nafuu jijini na kuleta ukuaji wa uchumi endelevu kwa wananchi na kuwa kichocheo baina ya Serikali na Sekta binafsi katika nyanja ya usafirishaji wa umma jijini.
Mwenyekiti wa Kamati ya DART, Dk Didas Masaburi ambaye pia ni Meya wa Jiji hilo, alisema wanatarajia kukihamishia Mbezi Luis kituo cha mabasi yaendayo mokoani na nje ya nchi ifikapo Januri 15, 2013 ili kupisha mradi huo wa DART.
 
Alisema kwa kuwa mradi huo ni wa wananchi, hivyo kuanzia sasa ushiriki wa madiwani na wenyeviti utapewa kipaumbele lengo likiwa ni kuwafikisha wananchi elimu kuhusu umuhimu wa mradi huo katika jamii.
Naye Diwani wa Kata ya Saranga (Chadema), Efraim Kinyafu alisema wakati ujenzi huo, bado hakuna juhudi za makusudi za kupanua barabara ili kuepuka foleni katika eneo la kimara hadi kituo kipya cha Mabasi Mbezi.
Mkutano umependekeza maazimio tisa yakiwemo ya, mkutano kati ya Meya wa Jiji na madiwani wa halmashauri kufanyika mara mbili kwa mwaka, kuundwa kamati itakayosimamia uandaaji sheria na kanuni zitakazo ongoza mamlaka hizo na mengineyo ambayo yatajadiliwa katika mkutano utakaofanyika hivi karibuni.
Akifunga Mkifunga Mkutano huo, Naibu Katibu Mku (Tamisemi), Jumanne Mgini, alisema viongozi hao wanapaswa kutambua kuwa suala la maendeleo yamo mikononi mwao, hivyo ni bora kila wanapojadili maendeleo ya jiji hilo wanafikisha ujumbe sasa hii kwa wananchi siyo vinginevyo.
 
Alisema suala la kuendeleza jiji hilo ni lao wenyewe hivyo wawe tayari kupokea machungu yatakayo ambatana na maendeleo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger