Pages

Home » » SERIKALI KUTUMIA WATAALAM WA KITANZANIA KATIKA KUTEKELEZA MIPANGO YAKE

SERIKALI KUTUMIA WATAALAM WA KITANZANIA KATIKA KUTEKELEZA MIPANGO YAKE


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye umuhimu kwa Taifa.
Hapo awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine, ambapo kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika pale tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi hawajapatikana kufanya kazi husika.
Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa Kitanzania kwenye maeneo yafuatayo:-
(i)Mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia  na mafuta.
(ii)Kuimarisha matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
(iii) Kuboresha utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha tunapata matokeo  makubwa na
ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.
Wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo haya, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha.
 
Mwito
unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ughaibuni au ndani ya
nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s) pamoja na maelezo ya kwa nini
wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta.

Tumia anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu Kiongozi
Ofisi ya Rais, Ikulu
S.L.P. 9120
DAR
ES SALAAM
.
E.mail:chief@ikulu.go.tz
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger