Pages

Home » » JK Afungua Mkutano Wa UVCCM Dodoma

JK Afungua Mkutano Wa UVCCM Dodoma

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa UVCCM, Benno Malisa alipowasili ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012

 Nderemo baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwasili ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012.
 Meza kuu na sehemu za wajumbe katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa UVCCM.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa UVCCM pamoja na ujumbe wa viongozi wa jumuiya za vijana toka nchi mbalimbali marafiki


 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa Chipukizi wa  UVCCM
NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, amenogesha Mkutano mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM unaoendea mjini  Dodoma.

Licha ya viongozi wengi kushangiliwa wakati wa kuingia ukumbini, nderemo na shamaramshamra zililipuka zaidi kutoka kwa wajumbe wa Mkutano huo wakati Nape alipotangazwa kuwasili.

"Jembe, jembe, jembe", wajumbe walisikika wakilipuka na kumshangilia baada ya Mkuu wa Umahasishaji na Chipukizi wa UVCCM, Esther Bulaya alipotangaza kuwasili kwa Nape ukumbini.

Ukumbi ulilipuka zaidi Nape alipopanda jukwaani na kuliungurumisha gita zito la besi, wakati Bendi ya Vijana Jazz ilipokuwa ikitumbuiza wimbo maalum, baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwasili ukumbini.

Viongozi wengine walioonyesha kuwakuna wajumbe wa mkutano huo wa vijana ambao ni wa Uchaguzi Mkuu ni pamoja, na Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma.

Baada ya mkutano kufunguliwa na Rais Kikwete, uchaguzi uliendelea ambapo leo, wanatarajiwa kupatika viongozi wapya wa UVCCM ngazi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Ujumbe wa Baraza Kuu UVCCM na wawakilishi kwenye jumuia zingine.

Katika nafasi ya Uwenyekiti ushindani ulihamia kwa wagombea wawili Msaraka Rashid Simai, Khamis Sadifa Juma baada ya mgombea mwingine Abdallah Lulu Mshamu kujitoa wakati wa kujieleza kwa wajumbe ukumbini.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wamechuana Ally Salum Hapi, Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita wakati nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti vitano Zanzibar wagombea 14, Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger