Picha hii aiendani na uhalisia wa tukio bali unashabihina na taarifa ya mkutano, samajhani kwa hilo mdau, huyo ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13 Oktoba, 2012 na Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo. Wengine pichani (kutoka kulia) ni Wajumbe wa Tume hiyo, Joseph Buti
Na Esther Macha, Mbeya
Imeelezwa kuwa sababu za kudorora kwa ujenzi wa hosteli za wanafunzi katika shule za sekondari Mkoani Mbeya, ni wananchi kukata tamaa ya kuchangia shughuli za maendeleo kutokana na kutosomewa taarifa za mapato na matumizi.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Bw.Modestus Dickson Kilufi kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri wa Mkoa(RCC) kilichofanyika jijini mbeya.
Bw. Kilufi alitoa kauli hiyo baada ya taarifa ya elimu ya mkoa wa Mbeya iliyowasilishwa ndani ya kikao hicho na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda, kuonyesha kuwa shule ya sekondari ya Madibira yenye kidato cha tano na sita iko hatarini kufungwa kutokana kukosa hosteli, hali inayosababisha wanafunzi kulala madarasani.
Alisema kuwa suala la wananchi kususia kujitoa katika kuchangia maendeleo hususani ujenzi wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi Mkoani hapo unatokana na utendaji na usimamizi mbovu wa viongozi wanaohusika kwa kutowasomea mapato na matumizi huku kukiwa hakuna jambo lolote linaloendelea baada ya kutoa michango yao.
Akitolea Mfano wa Shule ya Sekondari ya Rujewa Mbunge huyo alisema kuwa wananchi walijitoa kimasomaso kuchangia ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita muda mrefu lakini tangu wachangie michango hiyo hadi hakuna linaloendelea hadi sasa jambo ambalo alidai kuwa linachangia wananchi hao kukata tama ya kuchangia.
“Naomba ieleweke wazi kwamba wananchi siyo kusema kuwa hawataki kuchangia maendeleo ya ujenzi wa Hostel, tatizo lililopo ni kwamba wananchi wamekuwa wakichanga michango yao lakini wamekuwa hawasomewi mapato na matumizi huku kukiwa hakuna ujenzi wowote unaokuwa ukiendelea” alisema na kuongeza.
“Wananchi wapo tayari kuchangia maendeleo hayo lakini sumu iliyopo ni hiyo ya kutosomewa mapato ya matumizi ya michango yao, na kwamba hata kama wananchi hao ni wajinga kiasi gani kwa hilo hawata kuwa tayari kuendelea kujitoa kwa nguvu zao huku wasijue fedha zao zinakwenda wapi”alisema Mbunge huyo.
Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi.Hilda Ngoye alihoji uhalali wa kufunguliwa kwa shule hiyo ya Madibira wilayani Mbarali, wakati sera ya taifa ya elimu inaelekeza kuwa shule yenye kidato cha tano na sita ili ifunguliwe kigezo cha kwanza ni kuwepo kwa hosteli kwa wanafunzi wote.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro alionyesha kushtushwa na hoja hiyo na kuhoji kazi za kamati za maendeleo ya kata, pamoja na kuagiza wakuu wote wa wilaya Mkoani hapo kufuatilia na kuhakikisha taarifa za mapato na matumizi zinasomwa katika kila kijiji na yeye (Kandoro), kupewa nakala za taarifa hizo.

0 comments:
Post a Comment