WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amewataka wakulima wa kata ya Mwamapuli wakubaliane
kula njama na wakatae kuuza mpunga kutoka bonde la Rukwa ili wanunuzi
wote wanunue mchele badala ya mpunga.Alitoa rai hiyo jana jioni
(Alhamisi, Desemba 20, 2012) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya
Mwamapuli kwenye mradi wa mashine ya kukoboa mpunga akiwa katika siku ya
nane ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
Alisema kuuza mchele kutaongeza thamani ya zao hilo na
hivyo kufanya bei iwe juu. “Itabidi diwani na viongozi wengine wakae na
wananchi na kupanga bei ya kuuza mchele wao ili kuwa na sauti ya
pamoja,” alisema.
Alisema mashine hiyo ya kukoboa
ina uwezo wa kukoboa magunia 400 kwa siku kwa hiyo wana uhakika wa
kusindika kile wanachokizalisha.
Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa
jimbo la Katavi aliwaambia wakazi hao kwamba wafuate kanuni bora za
kilimo na kuwasisitiza kulima mpunga kwa kufuata mistari ili kuongeza
uzalishaji wa zao hilo kwa kila ekari.
Kesho (Jumamosi, Desemba 22,
2012) Waziri Mkuu atakuwa kata ya Kibaoni (kijijini kwao) ambapo
atazungumza na wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Kakuni.
WAZIRI MKUU ATOA SH. 5M/- KUHAMASISHA UFUGAJI NYUKI
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameahidi kutoa sh. milioni tano kwa wafuga nyuki 10
wa kijiji cha Mbede katika kata ya Mbede ili ziwasadie kutengeneza
mizinga ya kisasa.
Alitoa ahadi hiyo jana mchana
(Alhamisi, Desemba 20, 2012) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya
Mbede kwenye uwanja wa shule ya msingi Mbede akiwa katika siku ya nane
ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
Waziri Mkuu aliuliza kwenye
mkutano huo wa hadhara wangapi wana mizinga ya nyuki wakajitokeza watu
hao 10. Alipowahoji kila mmoja, alibaini kuwa jumla yao wote wana
mizinga 115 na zaidi ya mizinga 60 ina nyuki lakini akabaini kuwa wote
wanatumia mizinga ya asili ya kutundika juu ya miti.
“Nataka muanze kufuga kisasa… Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpanda itabidi usimamie zoezi la kutengeneza mizinga hii ili kikundi hiki kiwe kichocheo cha mabadiliko kwa wengine katika kata hii,” alisema.
“Achaneni na hiyo mizinga ya
asili kwa sababu uzalishaji wake ni mdogo, na kazi ya kuparamia ina adha
zake… kwenye mizinga ya kisasa unaweza kucheki nyuki kama wameingia
kwenye mzinga kadri unavyotaka,” alisema.
Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa
jimbo la Katavi aliwaambia wakazi hao kwamba nyuki wanaweza kufugwa kama
ilivyo kwa mifugo mingine. “Wanataka kuwekewa maji, mabanda yao
yanataka kusafishwa kila mara, na hii itakuwa rahisi kama tu mtatumia
mizinga ya kisasa,” alisisitiza.
Kesho (Jumamosi, Desemba 22,
2012) Waziri Mkuu atakuwa kata ya Kibaoni (kijijini kwao) ambapo
atazungumza na wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Kakuni.
WAZIRI MKUU AAHIDI KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameahidi kuchangia sh. milioni 20 za kuanzia ujenzi
wa kituo cha afya katika kata ya Mwamapuli ili kiweze kusaidia kata za
jirani za Mbede na Majimoto.Alitoa ahadi hiyo jana jioni
(Alhamisi, Desemba 20, 2012) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya
Mwamapuli kwenye mradi wa mashine ya kukoboa mpunga akiwa katika siku ya
nane ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
“Hapa Mwamapuli hatuhitaji tena
kuzungumzia habari ya zahanati sababu mmezungukwa na vijiji vingi na
kata nyingi. Mnahitaji kituo cha afya ili kata za jirani za Mbede na
Majimoto ziweze kunufaika,” alisema.
Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa
jimbo la Katavi aliwaambia wakazi hao kwamba wakimaliza kazi ya kuvuna,
waweke mpango mahsusi wa kuchangia matofali kwa kila kaya, na kila
kijiji ili kusaidia ujenzi wa kituo hicho.
Aliwasihi watendaji na wenyeviti
wa vijiji wasiwabugudhi wananchi kuhusu michango hiyo hadi
watakapomaliza msimu wa kilimo. “Tuwaache wamalize kuvuna ndipo
wachangie, tunataka kituo hiki kiwe kimefunguliwa ifikapo mwaka 2015,”
alisema huku akishangiliwa.
Pia aliwataka wafugaji na
wakulima wakae kwa kuheshimiana. “Wafigaji lazima tuendelee kuheshimu
wakulima, tusipeleke mifugo kwenye mashamba yao. Kuheshimiana ndiyo
kutatuondolea balaa la kupigana,” alisisitiza.
Kesho (Jumamosi, Desemba 22,
2012) Waziri Mkuu atakuwa kata ya Kibaoni (kijijini kwao) ambapo
atazungumza na wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Kakuni.
0 comments:
Post a Comment