Pages

Home » » WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU

WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU


 
 Na Heka Wanna na Shakila Galus,MAELEZO

MWENYEKITI wa WAMA Mama Salma Kikwete wito kwa wananchi tabia ya kujisomea vitambu na machapisho mbalimbali ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kujiletea maendeleo.

Mama Kikwete alitoa kauli hiyo kwenye Makumbusho ya Taifa    jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa makatba kwa ajili ya watoto na watu wazima.

 Alisema kuwa elimu ndio silaha pekee ya kukabiliana na maadui watu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini na hivyo kujiletea maendeleo.

Mama Kikwete aliongezea mbinu za kujiendeleza kimaisha zinapatikana pia kwa njia elimu kupitia  vitabu na machapisho mbalimbali yanayopatikana kwenye maktaba mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

 Alisema kuwa hiyo itasaidia katika kuongeza maarifa kwani kutakuwa na vitabu,kompyuta na mitambo ya mawasiliano ambayo itawawezesha watumiaji kupata elimu ya taaluma mbalimbali.

 Aidha Mama Kikwete aliwasihi watumishi wa Makumbusho hiyo kuwa ni jukumu lao kutunza maktaba hiyo ili isaidie kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuandaa taratibu bora za kudhibiti matumizi yasiyo na tija ya maktaba ikiwemo upotevu machapisho na vitabu mbalimbali  na uhalibifu wa vitabu unaofanywa na watu wasiotaka  maendeleo.

 Mwenyekiti huyo WAMA alimshukru Balozi wa Korea Kusini Young Shimo Dho kwa niaba ya nchi yake  kwa msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa ajili ya maktaba hizo mbili .
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger