Na Angelica Sullusi,Mbeya
Wajasiliamali nchini
wameiomba serikali kupandisha kodi kwa bidhaa zinazoingia nchini kutoka nchi za
nje hususani zile zinazofanana na bidhaa
zinazotengenezwa na wajasiliamali hao ili kulinda soko la bidhaa hizo nchini.
Ujumbe wa wajasilimali hao
umetolewa jana katika risala yao iliyosomwa mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara
ABDALAH KIGODA Jijini Mbeya jana katika Ufunguzi wa maonyesho ya wajasiliamali
Nyanda za Juu Kusini yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo
vidogo(SIDO).
Akisoma risala hiyo kwa niaba
ya wenzake Rhoida Mwazembe aliiomba serikali kuhamasisha watanzania kupenda
kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwa kutoa elimu kupitia vyombo vya
habari hususani kuanzisha vipindi vya kuelimisha jamii kupitia radio na
luninga.
Akijibu risala hiyo Waziri wa
Viwanda na Biashara Abdalah Kigoda alisema kuwa serikali inashughulikia tatizo
la upatikaji mgumu wa mitaji kwa wajasiliamali hao hususani kupata mikopo yenye
riba kubwa.
Aidha, Waziri Kigoda alitoa
agizo kwa Halmashauri zote za Wilaya nchini kuhakikisha zinatenga haraka maeneo
maalumu kwa ajili ya wajasilamali wadogo wadogo katika kuhakikisha wanapata
eneo maalumu la kuuzia bidhaa zao.
“Natoa agizo kwa Halmashauri
zote nchini kutenga maeneo maalum kwa wajasiliamali hawa ili kukabiliana na
changamoto wanayoisema ya kukosa mahali pa kufanyia kazi”alisema Kigoda.
Aliongeza kuwa serikali
inatambua umuhimu wa sekta hiyo kwa kuwa inakuwa kwa kasi hivyo
itajitahidi kuondokana na
nadharia na kufanya mambo kwa vitendo zaidi.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment