Na Angelica Sullusi,Mbeya
Vijana waishio katika Jiji la
Mbeya wametakiwa kujiunga pamoja pasipo kujali itikadi za dini,ukabila wala
vyama vya siasa katika kuhakikisha wanakabiliana na changamoto mbalimbali za
maisha.
Hayo yamesemwa jana na
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya
Dk.STEVEN MWAKAJUMILO katika hafla ya kufahamiana ya kikundi cha vijana wa
Forest Mpya iliyofanyika katika ukumbi mdogo wa hoteli ya Manyanya eneo la Forest.
Dk.Mwakajumilo alisema kuwa
kutokana na changamoto nyingi zinazolikabili taifa vijana hawana budi kujenga
mawazo ya kujiajiri kuliko kujibweteka kwa kutegemea serikali itawafanyia kila
kitu.
“Kupitia kikundi hiki tuanze
kujenga taswira mpya za kutafuta miradi mikubwa ili kuhakikisha kila kijana
anajitegemea kiuchumi katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa zima”alisema.
Aidha,aliwapongeza vijana hao
kwa kubuni mradi wa ufugaji kuku na kuwataka vijana wengine Jijini hapa kuiga
mfano kutoka kwa kikundi hicho.
Jumla ya shilingi milioni
mbili pamoja na ahadi zilichangwa katika kuimarisha mfuko wa kikundi hicho kwa
ajili ya maandalizi ya usajiri.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment