Pages

MBUNGE WA ARUSHA KUPITIA CHADEMA ASEMA KINANA AMEDANGANYWA NA WANACCM WENZAKE


Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwapokea viongozi wawili akisema wanatoka Chadema na kumtuhumu Mbunge wa Arusha, Godbless Lema kuwa anatumia madaraka yake kujinufaisha na mali za umma, mbunge huyo amejibu akisema: “Kinana amepigwa changa la macho.”


Akiwa Arusha mwishoni mwa wiki Kinana aliwapokea waliokuwa wenyeviti wa Chadema katika Wilaya ya Monduli, Amani Silanga na wa Ngorongoro, Revocatus Palapala lakini jana Lema alisema viongozi hao walikwishatimuliwa Chadema tangu mwaka 2013.

Kinana alisema migogoro ya CCM ndiyo iliyokinufaisha Chadema na Lema akaingia madarakani, lakini akawataka wananchi kujutia uamuzi huo na kutorudia kumchagua mbunge huyo.

“Mbunge wenu ameshindwa kutekeleza kile mlichomtuma bungeni badala yake anatumia madaraka yake kujimilikisha mali za umma na kutukana hovyo,” alisema na kuongeza:


“Mfano ni lile shamba alilopewa na Mayala ambalo ameliuza, trekta na vifaa vingine vyote ameviuza lakini migogoro ya ardhi na maji ameshindwa kuitatua.”

Majibu ya Lema

Akijibu tuhuma hizo, Lema alisema Kinana amepigwa ‘changa la macho’ na amefanyiwa maigizo kama ya futuhi na watu wa usalama wameshindwa kumwambia ukweli.


Alisema mambo yote aliyoambiwa ni uongo mtupu ambao yeye hawezi kusumbuka nao.


“Kama mimi ni mwizi na tapeli, hivi hata usalama wanashindwa kuwaeleza ukweli washughulike na mimi? Ndiyo maana watu tuliowafukuza Chadema wamewapokea eti wamehama chama. Wameingizwa mjini hao,” alisema.


Alisema: “Silanga na Palapala walifukuzwa tangu Novemba 30, 2013 baada ya kubainika kuwa kwenye mtandao wa Zitto na wote walitimkia ACT kama walivyofanya kina Mwigamba (Samson) na Kitila Mkumbo,” alisema Lema akitoa nakala ya taarifa kwa vyombo vya habari.

Alisema baadaye Silanga na Palapala walijiunga CCM na Palapala aligombea na kushinda uenyekiti wa Kijiji cha Wasso wilayani Ngorongoro kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba 14, mwaka jana.

“Ni maajabu ya mwaka mwenyekiti wa kijiji kupitia CCM tangu Desemba 14, mwaja jana, apokewe na Kinana akitangazwa kukihama Chadema?” alisema Lema.

Waziri Membe awaasa waimbaji wa nyimbo za injili nchini kuwa chachu ya amani na uadilifu nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb.) amezindua albamu mbili za nyimbo za injili zinazokwenda kwa majina ya "Pisha Mbele" na "Ni Ujumbe wa Bwana" za mwimbaji Mercy Nyagwaswa katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Machi, 2015. 
Askofu Mstaafu na Baba mzazi wa Mercy Askofu Nyagwaswa (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Mchungaji David Mangoti (wa pili kulia) na  Balozi Mstaafu Costa Mahalu wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi huo.  
Sehemu ya Wachungaji walioudhuria  uzinduzi wa albamu hiyo.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Bi. Mercy Nyagwaswa kulia akiwa na Mwimbaji mwenzake Bi. Upendo Nkone kwa pamoja wakimsikiliza Mhe. Membe ambaye  hayupo pichani alipozindua albamu zake za "Pisha Mbele" na Ni "Ujumbe wa Bwana". Wakati wa uzinduzi huo Waziri Membe alitoa rai kwa waimbaji wa nyimbo za injili nchini kuwa chachu ya amani na uadilifu ili nchi iendelee kuwa na utulivu na upendo. 
Mhe. Membe akiendelea kuzungumza
Bi. Mercy Nyagwaswa na kikundi chake akitoa burudani kwa mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi wa Albamu zake
Mhe. Membe na Askofu Mtaafu Nyagwaswa pamoja na wageni waalikwa wengine wakifurahia nyimbo zilizoimbwa na Bi. Mercy wakati wa uzinduzi wa album zake. 
Waziri Membe akikata utepe kuzindua  Albamu mbili za Bi Mercy Nyagwaswa.
Waziri Membe akimpongeza Bi. Mercy kwa kuandaag Albamu mbili kwa mara moja. 
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja.
Picha na Reginald Philip

LOWASSA AZIDI KUHAMASIKA JUU YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS, AWAHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWA WINGI DAFTARI LA WAPIGA KURA


Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais. 

Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu. Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.
 KIONGOZI WA MACHINGA MKOA WA DODOMA ALISEMA HAYA
 
RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI UDOM AKIZUNGUMZA.

LOWASSA ALIYASEMA HAYA KWA VIJANA HAO.
 Wanafunzi hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita mchana na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na kumchangia fedha za kuchukulia fomu.
Aidha Lowassa kwa Upande wake amewashukuru vijana hao na kusema kuwa ujio wao na ule wa masheikhe wa Bagamoyo unazidi kumhamasisha kutangaza nia na pindi muda ukifika anaweza kufanya hivyo.
 Walibeba na mabango yaliyo na jumbe mbalimbali
 Bodaboda nao walifika eneo hilo
Sehemu tu ya umati uliofika nyumbani hapo kwa Lowassa hii leo.

Dkt. Bilal afunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa Musoma


 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiambatana na wenyeji wake baada ya kuwasili mjini Musoma.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Mara Adam Ngalawa baada ya kuwasili mjini Musoma.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza wimbo wa Tanzania uliokuwa unaimbwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisangula.
 Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala, akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati), ramani ya Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma. Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.
 Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal kuzungumza na wananchi kwenye eneo la mradi.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akizungumza na wananchi.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu Aseri Msangi na kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Maghembe.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati) akikata utepe wa Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto kwake ni Balozi wa Ufaransa nchini, Melika Berak na viongozi wengine wa chama.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe  na katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak.

 Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Nadhifa Kemikimba akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia mifupa.
 Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Maji Kitaifa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba akizungumza na wananchi juu ya maadhimisho.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akimpa kikombe Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji wa Chuo cha Maji, Eng. Pantaleo Tumbo ikiwa ni moja ya zawadi zilizotolewa kwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Maji.

Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Musoma

Lee Kuan Yew afariki dunia





wakiweka mashada ya maua mbele ya hospitali aliyofia baba Lee Kuan Yew. 
 
Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia.Lee amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa mapafu.
Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha kimataifa.
David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini humo, ametuma salamu zake za rambi rambi.Kifo cha Lee ni mwisho wa zama zake.mwisho wa mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani katikati ya miaka ya sitini .
Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata leo na unaweza kuvuka mipaka sio kwa singapore tu bali hata kwa watu wa Asia ya kusini Mashariki.

Hofu ya Ebola Tanzania, mmoja ahofiwa


Mhudumu wa afya akiwa katika hali ya tahadhari ya Ebola huko Afrika Magharibi

Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Afya ya Tanzania Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika Magharibi ambaye ni mkazi wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Bwana Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo tayari ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari katika hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo.

Amesema sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini Benin.

Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania.

Taarifa hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya nchi hiyo kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa mmoja wa Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.

Chanzo:BBC SWAHILI

OFISI YA CHADEMA KATA YA RUAHA JIMBO LA IRINGA MJINI YACHUKULIWA NA CCM BAADA YA CHADEMA KUSHINDWA KULIPA KODI

IMG_9966 
Katibu wa CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu ( wa  pili  kushoto ) na kada wa Chadema aliyehamia CCM Ibrahim Mmasi  pamoja na  wanachama  wengine wa CCM wakiwa  wameshika bendera ya CCM ambayo itapepea katika ofisi mpya ya kata ya Ruaha ,ofisi ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na Chadema kabla ya  kufukuzwa kwa  kushindwa kulipa deni la kodi kiasi cha Tsh 540,000 , kushoto fundi rangi akiendelea  kupaka rangi ya CCM
IMG_9940Fundi akipaka rangi kuta za ofizi hiyo

………………………………………………………………..


CHAMA  cha  demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Ruaha  jimbo la Iringa  mjini kimepata  pigo  kubwa baada ya kufukuzwa katika nyumba  waliyopanga kama ofisi  ya kata  hiyo baada ya  kushindwa  kulipa deni la  pango  kiasi cha Tsh 540,000 walizokuwa  wakidaiwa na mwenye nyumba  deni  ambalo limelipwa  na Chama  cha mapinduzi (CCM ) kata ya  Ruahakabla ya  kuichukua ofisi  hiyo .
 
Mmiliki  wa nyumba  hiyo iliyopo mtaa wa Ngeleli Ipogolo Bi  Neema Mwasika alifikia  hatua  hiyo ya  kuwataka  kuondoka katika  ofisi  hiyo baada ya  jitihada za  kudai  deni lake  kushindikana na  hivyo kulazimika  kupangisha nyumba   hiyo yenye  chumba  kimoja na sebure  kwa  mpangaji mpya ambae ni CCM kata ya Ruaha.
 
Akizungumza na waandishi  wa habari  leo katibu  wa  CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu alisema  kuwa  awali CCM  kilikuwa na ofisi  yake  eneo la Ruaha  jirani na mto hivyo  kutokana na mvua  kubwa  zilizonyesha mwaka jana  zilipelekea  ofisi hiyo  kuharibiwa  vibaya na  hivyo  kukosa kabisa  ofisi .
 
Alisema kuwa  kutokana na kutokuwa na ofisi  cham a kilikuwa  kikitumia nyumba ya mtu binafsi kama  ofisi  pale ilipohitajika  kukutana  viongozi ama wanachama  .
 
Shungu alisema  kuwa jitihada za  kutafuta  nyumba ya  kupanga  ili  kutumika kama  ofisi ya muda ya  CCM kata  hiyo ya  Ruaha  ziliendelea kufanyika  chini ya aliyekuwa kada wa Chadema kata  hiyo kabla ya  kujiunga na CCM Bw  Ibrahim Mmasi
 
Hata  hivyo  alisema ofisi  hiyo alisema kuwa baada ya  kuona  ofisi  hiyo imefungwa kwa  muda na kuwasiliana na mwenye nyumba alikubali  kuwapangisha kwa makubaliano ya  kulipa deni kwanza jambo ambalo  lilifanyika  hivyo na kulipia kodi ya miaka  miwili zaidi.
 
” Tumeipata  ofisi  hii kihalali na sio hujuma kwani  makubaliano  kati ya mmiliki wa nyumba na mpangaji yalifanyika na  hivyo kwa  kuwa  hitaji letu  nyumba ya kupanga  tuliona  hiyo  ina  sifa ambayo tuliitaka  hivyo  tunachofanya ni kufuta rangi na nembo  za Chadema na kuweka rangi ya CCM na nembo  zetu …..na tutaizindua rasmi jumapili  wiki  hii”
 
Kwa upande wake  kada   wa CCM aliyehama kutoka Chadema Bw Mmasi  alisema  kuwa ofisi hiyo  ilikuwa imezinduliwa na viongozi wa  kitaifa  kupitia zoezi la oparesheni Sangara tarehe 19 mey 2011 chini ya  naibu mkuu wa Chadema enzi hizo Zitto Kabwe na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa na viongozi  wengine .
 
Chanzo:Fullshangwe
 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger