Jengo la shule ya sekondari ya Ufundi
Ifunda iliyopo katika Wilaya ya Iringa, "Ifunda Technical Secondary
School". Ambayo imesomwa na viongozi wengi wakubwa nchini, na wasanii
wenye majina makubwa ndani na nje ya nchi.
Wanafunzi wakiwa nje ya shule yao
Majengo haya kama yangefanyiwa japo
UKARABATI yangeweza kupendeza na hivyo kuvutia uwekezaji wa elimu kwa
vijana nchini na hata nje ya nchi, kwani shule hii ni maarufu na pia
niya wanafunzi wenye VIPAJI.
Jengo hili ni kama nembo "Logo" ya
shule ya sekondari ya Ufundi Ifunda, Limechoka, siku ya kushindwa
kuvumilia uchakavu huu wanafunzi wanaweza kupata madhara makubwa, kwani
jengo hili sasa ni chakavu mno.
Enzi hizoooo!! Hili lilikuwa ni Bus kwa
ajili ya kuwasafirisha wanafunzi, yaani ulikuwa ni usafiuri wa shule,
jamani leo hii lipo "Hoi bin taabani", Imebaki stori.
Magari haya nayo yalitumiaka
kusafirisha wanafunzi pamoja na kufanya shughuli mbalimbali za shule ya
sekondari ya ufundi Ifunda. Jamaaanii!!
Haya nayo nimajengo au tuyaite madarasa
katika shule yaa Ufundi Ifunda, enzi zake yalikuwa mazuri, sasa
kutokana na kukosa ukarabati yamezeeka.
Makamu mkuu wa shule ya sekondari
Ufundi Ifunda Bw. Shabani Nsute akisoma risala ya shule yake mbele ya
ugeni katika mahafali ya 12 ya kidato cha sita cha wanafunzi wa
sekondari ya Ufundi Ifunda Iringa.
Mmhhhh!!
Wanafunzi wahitimu wa elimu ya kidato cha sita sekondari ya Ufundi Ifunda wakisikiliza jambo katika mahafali yao.
Hiki ni choo, kwa wakati
huo kilikuwa nicha kisasa sana, kweli enzi hizo uwekezaji katika elimu
ulifanyika kwa kiwango kikubwa, shule kuwa na zaidi ya magari matano kwa
ajili ya wanafunzi na shughuli za shule siyo jambo la kitoto, leo hii
magari yote hayafai, na hivyo shule kutokuwa na gari hata moja la shule.
HABARI KAMILI
WALIMU na wanafunzi wa sekondari ya ufundi
Ifunda iliyopo katika Wilaya ya Iringa wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo kwa kushindwa kukarabati shule hiyo ambayo ni moja ya shule kongwe
hapa nchini.
Hayo yalizungumzwa na walimu na wanafunzi hao
katika mahafali ya 12 ya kidato cha sita na kuwa shule hiyo majengo yake
yamechaka na hivyo kupunguza ari ya wanafunmzi kupenda masomo.
Walisema shule hiyo imechakaa miundombinu yake
mingi kama umeme, maji pamoja na majengo yake yakionekjana kama magofu,
kutokana na kjuwa na umri mkubwa tangu tangu ianze kutumika mwaka 1950 kabla
nchi hii haijapata Uhuru.
Esther Mhode mwanafunzi wa shule hiyo yaUfundi
Ifunda, alisema majengo yake yanakatisha tamaa kuendelea na masomo,
kwani miundombinu ni mibovu hasa majengo ambayo ndiyo kivutio kikubwa kwa
wanafunzio kupenda masomo.
“Kama unavyoona majengo yetu utadhani ni
magofu, au majengo ya kumbukumbu, hali hii kwa kweli inachangia sana kushusha
hata kiwango cha ufaului waetu, kwani shule haina mvuto wa mwanafunzi kupenda
kujisomea, majengo nayo ni chachu kubwa katika kuboresha elimu, huwezi kuamini
hapa tunaambiwa wamesoma viongozi wakubwa na wasanii maarufu, lakini hawana
mchango wowote katika shule,”
Geofrey Nyamasagi muhitimu wa kidato cha sita
shuleni hapo, alisema endapo serikali ingeboresha majengo ya shule hiyo,
ingekuwa ni mfano wa kuigwa hasa kwa kuwa shule ni moja ya shule kongwe hapa
nchini.
“Humu ndani kuna mitambo ya ufundi imechakaa,
inaelekea zamani wanafunzi waliosoma katika shule hii walipata elimu sahihi, na
ndiyo maana wengi wao ni viongozi wa ngazi za juu ndani na je ya nchi,
shule niya vipaji malumu, lakini sasa kwa kweli imesahaulika mno, serikali
pamoja na wadau wa elimu hasa waliosoma katika shule hii wangefanyia
matengenezo ili kuifanya iwe endelevu,”
Wanafunzi hao walisema licha ya changamoto
hiyo ya miundombinu pia kuna uhaba wa walimu, hasa wa masomo ya ufundi, Sayansi
na Hisabati na hivyo kushindwa kupata elimu sahihi waliyokusudia, huku
changamoto nyingine kama upungufu wa vifa vya kujifunzia hasa kw masomo ya
Ufundi na Sayansi.
Naye makamu mkuu wa shule hiyo Shabani Nsute
alisema changamoto ya miundombinu ya maji inasababisha wanafunzi kutumia muda
mwingi kuacha masomo na kwenda kuchota maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya
shule.
Nsute alisema uchakavu wa miundombinu ya shule
husababisha wanafunzi kuacha masomo na kwenda kuchota maji ya kupikia na
matumizi ya vyoo ambavyo vilijengwa kwa mfumo wa matumizi ya maji mengi.
Alisema hata nyumba zao walimu ni chakavu
licha ya shule hizo kulipa kodi, lakini hazijawahi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote
kwani na kuwa awali ilianza kama chuo cha ufundi (Ifunda Trade School)
mwaka 1950 na mwaka 1964 chuo kilibadilishwa na kuwa shule ya sekondari ya
ufundi.
Ofisa elimu taaluma sekondari Wilaya ya Iringa
Devotha Luwungo alisema ili kukabiliana na changamoto za shule hiyo, serikali
imeanza kutoa shilingi Miliono hamsini kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya
shule kongwe, na sasa fedha hizo zitaelekezwa katika shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment