Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Job Masima akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima Ofisini kwake leo alipomtembelea na wajumbe kutoka JWTZ Makao Makuu waliofika Mkoani Rukwa kwa ajili ya kujionea shughuli zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni kuzoa shehena ya mahindi kutoka Mkoani Rukwa kwenda Mkoa jirani wa Katavi ambapo yatasafirishwa kwa reli kwenda Mikoa ya Kaskazini. Jumla ya tani 20,000 zinategemewa kusafirishwa na jeshi hilo ambapo mpaka sasa zimeshazolewa tani 11,000. Mahindi hayo yamenunuliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Chakula.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza na ugeni huo Ofisini kwake. Akizungumza katika kikao hicho Alhaj Chima alilishukuru jeshi hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya kwani mpaka sasa hakuna malalamiko yeyote yaliyojitokeza.
Baadhi ya maofisa wa jeshi hilo waliongozana na Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Samson Mashalla
0 comments:
Post a Comment