Afisa
Utafiti Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bwana Emphraim Mdee
akiongea na Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Urasimishaji wa Tasnia ya
Filamu na Muziki Tanzania na kuanzishwa kwa utaratibu wa kubandika
stempu za kodi kwenye kazi za wasanii,katikati ni Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo.(Picha na Benjamin
Sawe wa WHVUM).
……………………………………………………………..
Na Heka Wanna na Shakila Galus-MAELEZO_ Dar es salaam
Serikali imeeleza kuwa kuanzia Januari mosi mwakani (2013) itaanza kubandika stempu za kodi katika bidhaa za filamu na muziki.
Hatua
hiyo inalenga kuwasaidia wasanii wa filamu na muziki kupata mapato ya
kazi zao na kuweka mfumo mzuri wa namna ya kudhibiti wizi wa kazi zao
kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania
Kauli
hiyo ilitolewa na Afisa Utafiti Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania Ephraim Mdee alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana
jijini Dar es salaam.
Alisema
kuwa TRA kwa kushirikiana na wadau wengine wataanza kubandika stempu za
kodi(Tax Stamps)ambazo zitakuwa maalum ili kusaidia usimamizi na
udhibiti wa kazi za wasanii ambazo zitawekwa katika DVD, CD, na Tape.
Mdee
aliongeza kuwa kazi za wasanii ambazo tayari ziko sokoni zitakiwa
zirudishwe kwa ajili ya kubandikwa stempu na kuongeza kuwa zoezi la
kurudishwa litafikia ukomo Mwezi Julai mwakani.
Alisema kuwa baada ya hapo mtu atakayekutwa akiuza kazi ambazo hazina stempu ya kodi atachukuliwa hatua ya kuvunja sheria.
Hivyo ametoa wito kwa wasambazaji wote kukusanya kazi ambazo wamezipeleka sehemu mbalimbali kabla ya Julai mwakani .
Aidha
alisema kuwa TRA pia itanzishwa mfumo wa pamoja wa kieletroniki wa
mawasiliano ambao utaunganisha taasisi zote zinazo husika na tasnia ya
filamu na muziki ili kuhakikisha kuwa taarifa za wadau au wasanii
zinapatikana kwa uhakika na usahihi
Alitoa
kwa wananchi wote kuhakikisha kuwa wanashiriki katika
kulinda,kuthamini na kuendeleza tasnia za filamu na muziki kwa kununua
bidhaa zilizowekwa stempu za kodi
0 comments:
Post a Comment