(NA JOEL MWAKABUNGU -SUMBAWANGA)
Katibu mkuu wa Wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bw.Job Masami alitembelea mikoa ya Katavi na Rukwa kwa
ajili ya kutembelea na kukagua maendeleo ya shughuli ya uhamishaji wa shehena ya mahindi kutoka mjini Sumbawanga
mkoani Rukwa na kupelekwa mjini Mpanda mkoani Katavi, shughuli inayofanywa na malori yanayomilikiwa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania JWTZ.
Alielezwa kuwa hadi sasa zaidi ya tani 11,600 za mahindi zimeshahamishwa kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda kwa ajili
ya kusafirishwa kupelekwa kwenye Kituo cha Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa NFRA cha mkoani Shinyanga, na kwamba
ni jumla ya tani 20,000 za mahindi ndizo zinazotakiwa kuhamishwa kutoka Sumbawanga kwenda Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana
na suala zima la njaa kwenye maeneo hayo ya kanda ya ziwa.
Alipata fursa vile vile kuongea na makamanda wa Jeshi hilo la ulinzi zmbalo lina malori 65 hadi sasa mkoani Rukwa na Katavi
yanayohamisha mahindi hayo, na kwamba wana mpango wa kuongeza malori mengine 50 ili kuharakisha uhamishaji wa
shehena hiyo ya mahindi, wakilenga kuukimbia msimu wa mvua unaokaribia kuanza, kwani mara kwa mara mvua zinachangia
kuharibu miundo mbinu.
0 comments:
Post a Comment