Hatimae
Nahodha wa Chelsea John Terry ameamua kutokata Rufaa kupinga Adhabu
yake ya kufungiwa Mechi 4 na Faini ya Pauni 220,000 baada ya kupatikana
na hatia na FA, Chama cha Soka England, ya kumkashifu kibaguzi Beki wa
QPR Anton Ferdinand.
Uamuzi huu wa Terry, ambao umekuja
katika Siku ya mwisho ya yeye kutakiwa akubali au apinge adhabu yake,
unamaanisha atazikosa Mechi za Klabu yake Chelsea za Ligi Kuu England
dhidi ya Tottenham, Manchester United na Swansea City na pia Mechi ya
CAPITAL ONE CUP dhidi ya Man United.
Tukio lililomsulubu Terry lilitokea
Oktoba 23 Mwaka jana huko Uwanja wa Loftus Road kwenye Mechi ya Ligi
ambayo QPR iliifunga Chelsea bao 1-0.
Baada ya hapo Kesi hiyo ilitinga
Mahakamani baada ya Shabiki mmoja kupeleka malalamiko Polisi lakini
Mwezi Julai Mahakama ya Westminster ilimwachia huru na hapo ndipo FA
ikaamuru Jopo lake Huru la Nidhamu lisikilize Kesi hiyo na ndipo ikamtia
hatiani baada ya kutoukubali utetezi wake.
Akikubali adhabu yake, Terry Miaka 31, amesema: “Naomba nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa kila mtu kwa lugha niliyotumia.”
Pia aliongeza: “Ingawa nimehuzunishwa na
hukumu ya FA, ninakubali kuwa lugha niliyotumia, ukiachilia mbali
mazingira yake, haikubaliki kwenye Uwanja wa mpira au popote pale
maishani. Kama nilivyosema Mahakamani, ningekuwa najua nini kitatokea,
lugha niliyotumia ni wazi haikufaa kwa Mtu wa nafasi kama yangu. Uamuzi
uko chini ya kile Klabu ya Chelsea inataka na kwangu pia na hili
halitarudiwa tena.’’
Hadi sasa Klabu ya Chelsea haijatoa
tamko itamchukulia hatua gani Terry mbali ya kusema inasubiri uamuzi wa
Terry kama atakata Rufaa au la.
0 comments:
Post a Comment