Na ESTER MACHA, Ileje.
UBOVU wa bara bara katika Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya umesababisha
hali za maisha za wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa duni
kutokana na kushindwa kusafilisha mazao wanayolima kwenda mikoa
mingine.
Akizungumza na mwandishi watu
ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi.Rosemary Senyamule alisema
hayo kufuatia ubovu huo wa bara bara ambao umedumu kwa muda mrefu bila
jitihada zozote za kuhakikisha kuwa zinatengenezwa ili wananchi waweze
kuwa na hali nzuri za kimaisha.
Alisema kuwa ubovu huo wa bara bara umekuwa ni tatizo kubwa kwa
wananchi na hata kushindwa kushindwa kusafilisha mazao na vitu vingine
ambavyo ni mkombozi kwa wananchi ambavyo vingeweza kuokoa hali za
maisha.
“Hili suala la miundo mbinu katika wilaya hii ni tatizo kubwa sana
ambalo linasababisha uchumi wa wananchi wa wilaya hii kuendelea duni
,ili kuweza kufanikisha hili serikali inaendelea kufanya jitihada ili
kuhakikisha kuwa miundo mbinu hii inatengenezwa mapema”alisema.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema hilo likifanikisha hali ya uchumi kwa
wananchi itaweza kubadilika haraka na wanancghi kuweza kufanya kazi zao
kwa mara moja ,hivi sasa safari ya kutoka Mpemba Ileje mwananchi
anatumia masaa matatu mpaka manne wakati ni safari ya saa moja tu.
Aidha Bi.Senyamule alisema kama serikali wanaendelea na na jitihada
aza kuhakikisha kuwa bara bara hiyo inatengenezwa na kupewa kipaumbele
kwenye bajeti ijayo .
Mmoja wa wananchi wa Tarafa ya Kipambawe Wilayani hapa Bw.Sifanuel Luka
alisema kuwa tatizo la kutokuwa na bara bara nzuri katika wilaya hiyo
limekuwa ni shida kubwa kwao kwa kushindwa kusafirisha vitu muhimu kwao
ambavyo vingeweza kuondoa ugumu wa maisha.
“Kwa ujumla hili ni tatizo kubwa sana sehemu ya kwenda na kurudi
inakulazimu mpaka ulale kwa hali hii maisha lazima yawe magumu kwa
sisi wananchi,wilaya hii ni muda mrefu hebu angalia maisha ya wananchi
wa wilaya hii walivyo na maisha magumu serikali ifanye jitihada mapema
kuhakikisha kuwa bara bara hii inatengenezwa haraka”alisema.
0 comments:
Post a Comment