FFU
Akijibu hoja za waamini.wameomba wapewe ulinzi na serikali iwajibike kujenga kanisa kwani polisi walizembea kuzuia waislamu waliokuwa wakifanya vurugu kwa awamu tatu bila polisi kudhibiti hali hiyo
Kamanda wa mkoa wa Temeke
Yupo kazini
Askofu Malasusa Awatuliza Wakristo Mbagala
Askofu
mkuu wa KKKT Alex Malasusa akiwaasa wakristu kuwa watulivu wakati huu
wakati mamlaka za dola zikishughulikia swala hili,wakati huu wadumu
katika maombi na wawasamehe ndugu zao waislamu. na kuwaombea.Mungu
atawapigania
Uharibifu Uliosababishwa Na Waislamu Mbagala
waumini wakiwa katika maombi na huyu akilia kwa uchungu
Mchungaji
wa TAGP akiongoza maombi wakristo wakiwaombea waislamu.Mpaka muda huu
hakuna kiongozi yeyote wa serikali ameshafika eneo la matukio na uongozi
wa kanisa unawasubiria viongozi wa kiserikali
Katika madhabahu, pameharibiwa
Mabenchi yamepinduliwa na kuvunjwa
Mimbari imechomwa na kuharibiwa
Ofisi ya Kanisa imechomwa moto
Wachungaji wa kanisa hili wakisubiria taarifa kutoka polisi
Hawa wanafanya maombi na nimesikia wakiwaombea Waislamu Mungu awasamehe
Vifaa vya uimbaji vimechomwa moto
Washarika wakiwa kanisani kwao asubuhi hii
Gari la mchungaji pia limeharibiwa kabisa
Ofisi ya mchungaji na mwinjilisti zimeharibiwa kabisa
Kushoto ni msikiti walipotokea Waislamu kabla ya kuvamia kanisa kulia. Nyumba hizi za ibada ziko jirani zikitenganishwa na barabara tu
Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Jana Ijumaa tarehe 12
Agosti 2012, jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam Tanzania lilipata kazi ya
ziada ya kutulia ghasia baada ya kijana mmoja wa Kikristo anayejulikana kwa
jina la Emmanuel Josephat kuutemea mate na kuukojolea Msahafu huko Mbagala na
hivyo kuamsha hasira za Waislamu wenye uchungu na dini yao.
Polisi wametua mabomu
ya machozi kuwatawanya Waislamu wenye hasira ambao walikuwa wanataka polisi
iwakabidhi kijana huyo aliyeivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Makanisa kadhaa
yamechomwa moto baada ya polisi kukataa kuwakabidhi Waislamu kijana huyo
aliyevunjia heshima matukufu ya dini yao tukufu.
Taarifa zinasema kuwa
polisi wanawashikilia zaidi ya Waislamu 100 kufuatia ghasia hizo. Waislamu
wanaendelea kushinikiza kuachiliwa huru wenzao hao.
Juhudi za viongozi wa
Kiislamu za kujaribu kuwatuliza Waislamu zilishindwa jana licha ya viongozi hao
kuafikiana na Polisi kushirikiana kutuliza hali ya mambo.
Bwana Hamis Salum
Mzazi wa kijana ambaye alipokonywa Msahafu huo amenukuliwa akisema: Kijana
wangu alikuwa anatoka Madrasa alipofika katika maeneo ambayo huwa wanapenda
kucheza mpira akaja huyu kijana akamwambia wewe una mapepo, hii Qur'ani ni kitu
gani, mnapoteza muda tu, kule kuna mashetani, majini na uchawi... halafu yule
kijana akachukua Msaafu akaufunua wakatokea watoto wengine wakamwambia
utadhurika, utageuka mjusi... akaufunua na kuutemea mate na kisha baadae
akaukojolea"
Polisi wameripoti
kutumia nguvu za ziada zilizowakumba hata wasio Waislamu.
0 comments:
Post a Comment