Na Veronica Kazimoto – MAELEZO Dar es Salaam 18.10.2012
Sikukuu ya Eid-El-Hajj itakuwa siku ya tarehe 26 Ockoba mwaka huu ambapo kitaifa swala itafanyika katika msikiti wa Vuchama wilayani Mwanga katika mkoa wa Kilimanjaro ikifuatiwa na Baraza la Eid baada ya Swala.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa habari na mawasiliano ya Umma Simba Shabani wa Baraza Kuu la Waislam wa Tanzania (BAKWATA) mgeni rasmi anatarajiwa kuwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa sababu ya tarehe hiyo ni kutokana na siku hii ya leo kuwa mwezi pili, Dhul-Hijja mwaka 1433 kwa mujibu wa kalenda ya Kiislam.
Aidha Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Issa Bin Shaaban Simba amewataka Waislam wote nchini kusherehekea kwa amani na utulivu sikukuu hiyo huku wakichunga mipaka ya Allah (S.W).
Sheikh Shaaban Simba pia amewataka waislamu kutii sheria za nchi na kuepukana na watu ambao wanataka keleta tafrani za kidini hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment