Makao makuu ya ofisi za mradi wa umeme Matembwe Lupembe.
Zaidi ya Kaya Elfu 20 za Tarafa ya Lupembe Mkoani Njombe zinatarajia Kunufaika na Mradi wa Umeme wa Nguvu ya Maji Kutoka Chanzo cha Mto Ikondo Utakaozalishwa na Matembwe Villege Company Limited Ifikapo Mwaka 2014.
Akizungumza na MTANDAO HUU Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Hiyo Bwana Yohanis Kamonga Amesema Hadi Hivi Sasa Tayari Zaidi ya Wakazi 720 Zikiwemo Taasisi za Serikali na Zisizo za Kiseriklai za Kata ya Matembwe Zimepatiwa Umeme Unaozalishwa na Kampuni Hiyo Kutoka Chanzo cha Mto Nyave Kilichopo Kata ya Matembwe.
Aidha Mkurugenzi Huyo Mtendaji Amesema Kuwa Umeme Utakaozalishwa Kutoka Chanzo cha Mto Ikonda Utatoa Kilowatt Mia Nne , Ambao Utaonganishwa na Umeme wa Kilowatt 120 Kutoaka Chanzo cha Mto Nyave Uonatumika Hivi Sasa Ili Kuongeza Nguvu.
Kwa Upande Wao Wakazi na Wadau wa Maendeleo Tarafa ya Lupembe
Wamelipongeza Kampuni Hilo Kwa Kuwasongezea Huduma ya Nishati Umeme na
Kusema Kuwa Mradi Huo Utawapunguzia Tatizo la Upatikanaji wa Umeme wa
Uhakika Unaowakabili Kwa Sasa Wakazi wa Tarafa Hiyo
Takribani Vijijini Saba Vya Tarafa ya Lupembe Vinataraijia Kunufaika na Mradi Huo Huku Vijiji Vilivyo na Nishati ya Umeme Vitapata Fursa ya Kufungiwa Njia Nyingine za Umeme.
0 comments:
Post a Comment