MILIONI
sita zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Selemani Said (1),
ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku ukiwa nje ya
tumbo lake imeleezwa.
Akizungumza na wandishi wa
habari Katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini Dar es Salaam
leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent ambaye ni Mkazi wa Bunju,
alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na sehemu ya kutolea haja kubwa
lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa ikitokea mdomoni.
Alisema msaada wa fedha hizo
utasaidia katika kumfanyia operesheni mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi
akiwa katika mateso makubwa.
Veronika alisema hivi sasa yeye
pamoja na mwanaye huyo wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya baba wa
mtotohuyo kuitelekeza familia hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto
huyo.
“Mimi ni nachoomba ni msaada wa
fedha ili niweze kumpeleka kwenye matibabu kwani sina msaada
wowote,ukichukulia wazazi wangu kufariki na hivi sasa naishi kwenye
nyumba ya mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju wilayani Kinondoni jijini baada
ya kushindwa kupangisha chumba kwani sina kazi yeyote”alisema.
Aidha, alisema hadi utumbo wa
mtoto huyo kutoka nje, ni baada ya kufanyiwa operesheni katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili ambapo hata alipompeleka tena kwa ajili ya
matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa madaktari na wahudumu wengine.
Alisema kwa yeyote ambaye yuko
tayari kumsaidia anaweza wasiliana naye kwa kupiga simu namba o715 83 77
00, na namba ya mwenyekiti huyo wa mtaa 0656780236.
Veronika ni mzaliwa wa Mkoa wa
Kilimanjaro eneo la Kijiji cha Uru,Moshi ambye alimzaa mtoto huyo na
mwanamme aliyemtaja kwa jina la Abdalah Said, kabilake makonde
mfanyabiashara wa viatu Ubungo.
0 comments:
Post a Comment