Home »
» BABA ANAETUHUMIWA KUZINI NA KUZAA NA MWANAE WA KUMZAA ATINGA MAHAKAMANI BAADA YA KESI KUAIRISHWA AZOMEWA NA KINA MAMA NA KUKIMBIA KAMERA ZA WANDISHI WA HABARI
BABA ANAETUHUMIWA KUZINI NA KUZAA NA MWANAE WA KUMZAA ATINGA MAHAKAMANI BAADA YA KESI KUAIRISHWA AZOMEWA NA KINA MAMA NA KUKIMBIA KAMERA ZA WANDISHI WA HABARI
|
Mkazi
wa Mtaa wa Mbete,Kata
ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba
binti
yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo
mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao
tumefunika
|
|
Bwana
Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera
mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha |
|
Jamaa
kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno
makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari
hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo |
|
Huyoooo anatoka nje ya mahakama |
|
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi |
|
Njooni sasa huku kashika jiwe |
|
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku akiwa na jiwe lake mkononi |
|
Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata
ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti
yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi
wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu
kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa
Balozi wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa
Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa
walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa
alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba
alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo
kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo
Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa
daktari ambaye
alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.
Binti
huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo
kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe
12/12 mwaka huu,
|
0 comments:
Post a Comment