Kipande
cha barabara ambacho ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami kati
ya Ndundu mkoani Pwani na Somanga mkoani Lindi chenye urefu wa kilometa
60 sasa umepangwa kukamilika kabla ya mwezi Juni 2013. Taarifa hiyo
imetolewa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mhe. Eng. Gerson
Lwenge wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete alipotembelea mradi huo akitokea mkoani Lindi.
Mheshimiwa Lwenge alimjulisha Rais Kikwete kuwa, baada ya mkandarasi
huyo kushindwa kuikamilisha kazi hiyo mwezi Januari 2011 kwa mujibu wa
mkataba, taratibu kadhaa zilifuatwa ili kuhakikisha kuwa mkandarasi huyo
anachukuliwa hatua stahiki kwa lengo la kuhakikisha anaikamilisha
kilometa 28 zilizobaki kama ilivyokusudiwa.
“Hatua kadhaa zimekwishachukuliwa ambapo kwa sasa mkandarasi ameweza
kuongeza uwezo kwa kuzalisha kilometa 5 za lami kwa mwezi na hivyo
kurudisha matumaini kuwa ndani ya miezi sita kazi hiyo inaweza kuwa
imekamilika” alisema Naibu Waziri Injinia Lwenge..
Mheshimiwa Rais aliitaka Wizara ya Ujenzi kupitia Tanroads kuhakikisha
kuwa inausimamia mradi huo kwa karibu zaidi ili kuondoa visingizio
vingine vyoyote vinayvyoweza kusababisha mradi huo kuchelewa zaidi.
Ujenzi wa sehemu hiyo ya barabara ambayo ndiyo pekee iliyobaki katika
barabara kuu inayounganisha mikoa ya Kusini na Jiji la Dar es Salaam,
ulianza mwaka 2008 ukiwa umepangwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.
Mkadarasi aliyeshinda zabuni hiyo ni Kampuni ya M/S M.A. Kharafi &
Sons kutoka Kuwait kwa gharama ya Shs. 58.8 bilioni. Fedha hizo
zimetolewa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na mifuko ya
maendeleo ya KUWAIT na OPEC.Baada ya ziara hiyo Mheshimiwa Rais alirejea
Dar es Salaam.
NEW VIDEO:- CHRIS BEE - SIENDI MBALI
6 years ago
0 comments:
Post a Comment