NAIBU
Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu, amesema serikali kuanzia
sasa itawakamata baadhi ya watu waliyojianzishia viwanda bubu
vinavyozalisha bidhaa hafifu nchini.
Kauli hiyo ilitolewa, na waziri
huyo wakati alipotembelea viwanda vinavyomilikiwa na Kampuni ya MMI
Steel Mills Limited vilivyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam jana.
Alisema lengo la kuwakamata watu hao ambao wamo hata wageni ,
na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ni kudhibiti bidhaa hizo kwenye
soko ambapo zimekuwa zikiwatia hasara wananchi pia kuviharibia sifa
baadhi ya viwanda.
Teu alisema viwanda hivyo
vimekuwa vikiiga bidhaa kama nondo na mbati, kutumia nembo za kampuni
mbalimbali zinazotambulika nchini kama vile MMI Steel Mills Limited.
Alisema kutokana na ubabaishaji
huo unaofanywa na baadhi ya watu, serikali itahakikisha inazisaidia
kampuni zote zilizoanzishwa kwa kufuata sheria.
“Kampuni hii ya MMI Steel Mills
imekuwa kwa muda mrefu ikitoa mchango mkubwa katika kuchangia pato la
taifa haswa kwenye eneo la kodi pia imepanua wigo wa ajira kwa
Watanzania ambapo pia kimekuwa kikiingizia Tanesco jumla ya sh. bilioni 1
kama bili kwa mwezi ”alisema Teu.
Akizungumzia kuingiliana kwa
mipaka kati ya Kiwanda hicho na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC
katika mradi wa kutengeneza chuma cha Liganga na mkaa wa mawe huko
Katewaka, Teu alisema, hata yeye utata huo umemshtua sana.
Alisema matatizo hayo
yamesababishwa utoaji wa zabuni, kutokana na upande mmoja kutokuwa
makini ambapo pia aliwaomba wasichoke, watalifanyia kazi kama wizara.
Awali Mhandisi, Raulence Manyama viwanda hivyo vya chuma, vilikuwa vikikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa chuma.
Alisema hadi kufikia mwa 2012
kulikuwa na viwanda na viwanda 21 vya chuma nchini vyenye uwezo wa
kuzalisha zaidi ya tani 200,000 za chuma kwa mwaka.
Aliasa serikali kuongeza uwezo
nchi kuzalisha aina nyingi ya bidhaa ya chuma ambazo kwa sasa zinatoka
nchi za nje, hizo ni hot-roll coils, cold coils, flat bars na aina
nyingi za chuma.
0 comments:
Post a Comment