Na.Mwandishi wetu
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMAN
amesema jeshi la polisi limekuwa likilazimika kutumia shuruti kwa madereva wa
daladala kutokana na madereva hao kutofuata sheria zilizopo.
Akiongea na mwandishi wetu kamanda ATHUMAN amesema
mamlaka ya kudhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) hawatasita
kuwachukulia hatua madereva wazembe.
“Kila mtu anatakiwa kufuata sheria na mtu yeyetote
ambaye atafanya kosa asitegemee kama atasamehewa kwa uzembe wake, na kwa mtu
yeyote ambaye atakatisha ruti hatua kali za kisheria, pia wamilikiwa wa magari
wahakikishe madeeva wao wanafuata utaratibu ikiwa ni pamoja kutopandisha nauli
kwa daladala ziendazo Mbalizi na ruti kuishia Sae badala ya uyole Dereva
atachukuliwa hatua mara moja bila huruma yoyote”Alisema Kamanda ATHUMAN.
Wakati huohuo amewataka wakazi wa mkoa wa Mbeya
kutojihusisha na vitendo vya vurugu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi
la polisi dhidi ya wote ambao wanahatarisha amani ya nchini
“Usalama ni eneo muhimu la kulipa kipaumbele endapo
tutakuwa tumedhamiria kufikia malengo yetu katika shughuli mbalimbali, pia
vitendo vya vurugu vinakwamisha maendeleo kwa wawekezaji kuingiwa na hofu ya
kuwekeza mkoani hapa”
Kuhusu suala la askari kulazimisha madereva kutoa
rushwa barabarani amesema dawa imekwisha patikana na tatizo hilo linaweza
kumalizika kwa ushirikiano kati ya Jeshi lake, wananchi na waandishi wa habari
0 comments:
Post a Comment