CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimewafungia wachezaji
wake wote waliokuwa katika kikosi cha timu ya taifa (Zanzibar Heroes)
ambao walikuwa wakishiriki michuano ya CECAFA Tusker Chalenji. Wachezaji
hao wamefungiwa kucheza soka ndani na nje ya nchi na kutakiwa kurejesha
fedha zote za zawadi ya Dola 10000 za msindi wa tatu walizopokea nchini
Uganda na kuamua kugawana wenyewe bila kushirikisha uongozi.
Kwa mujibu wa taarifa ya ZFA waliofungiwa ni:- makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud ‘Chollo’ (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali ‘Canavaro’ (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Wengine ni viungo; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende
Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman
Kassim ‘Selembe’ (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars),
Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black
Sella), Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ (Azam) na washambuliaji; Amir Hamad
(JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri),
Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).
0 comments:
Post a Comment