Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Mhe. Aggrey Mwanri akikagua mradi wa maabara katika kituo cha
afya cha Matai katika Wilaya mpya ya Kalambo leo. Naibu Waziri huyo
amepiga marufuku miradi yote ya serikali hususani inayohusisha mbao
kupigwa rangi na badala yake ipakwe vanish, hiyo ni kutokana na baadhi
ya wakandarasi kutumia staili hiyo kuiibia Serikali kwa kuweka mbao za
bei nafuu na kuzipiga rangi. Mhe. Mwanri yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya
kikazi ya siku saba ambapo ataembelea halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa
na kukagua miradi mbalimbali iliyopo chini ya Halmashauri hizo.
Naibu
Waziri TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) akikagua ujenzi wa banio la
mradi wa umwagiliji katika kijiji cha Katuka katika Halmashauri ya
Wilaya ya Sumbawanga. Mhe Mwanri aligoma kuweka jiwe la msingi katika
mradi huu kutokana na mkandarasi kujenga mradi huo chini ya kiwango
kinyume na mchoro halisi wa mradi huo. Aliagiza mapungufu yarekebishwe
ndipo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a aweke jiwe hilo kwa niaba
yake.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Mussa Chang’a akimkaribisha Mhe.
Mwanri azungumze na wananchi wa Wilaya ya Kalambo katika ziara yake
ambayo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutumia fursa ya miundombinu
inayoendelea kujengwa Mkoani Rukwa pamoja na ujio wa Halmashauri yao
mpya katika kuwekeza na kujiendeleza kiuchumi.
Kutoka
kushoto ni Mama Mwanri mke wa Naibu Waziri, Mhe. Agrey Mwanri Naibu
Waziri TAMISEMI, Mhe. Moshi Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Kalmabo na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Godfrey Schona wakiwa
katika picha ya pamoja pembezoni mwa fukwe za Ziwa Tanganyika katika
Hoteli ya Liemba Beach Resort walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara
yake Mkoani Rukwa.
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika
nyumba ya mganga wa kituo cha afya Matai mapema hii leo. Katika miradi
miwili aliyotembelea Mhe. Mwanri aligoma kuweka mawe ya msingi hadi hapo
marekebisho aliyoagiza yatakapofanyiwa kazi ndipo mawe hayo yawekwe kwa
niaba yake.
Mama Mwanri akiwasalimu wananchi wa Matai katika Wilaya ya Kalmbo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akiwasalimia wananchi
wa kijiji cha Kipeta kabla ya Mhe. Mwanri kuzungumza nao kwenye ziara
yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo Mkoani Rukwa.
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Ndugu Agrey Mwanri akipanda kwa tahadhari kubwa
katika daraja la Mto Momba linalounganisha wananchi wa Kilyamatundu
Mkoani Rukwa na wale wa Kamsamba Mkaoni Mbeya. Daraja hili lililojengwa
kwa kamba limekuwa halikidhi haja ya wananchi hao jambo wanaloomba
Serikali kuwajengea daraja litakalowawezesha kuvuka na kuvusha mazao yao
kirahisi.
0 comments:
Post a Comment