Pages

Home » » MTANGAZAJI ALIYEPOTEA AKUTWA AMEKUFA PORINI NA KUTOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI

MTANGAZAJI ALIYEPOTEA AKUTWA AMEKUFA PORINI NA KUTOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI

Bw. Issa Ngumba.
Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera anayefanyia kazi wilayani Kakonko mkoani Kigoma Bw. Issa Ngumba aliyepotea katika mazingita tata amekutwa amekufa na kunyofolewa  sehemu zake za  siri
 
Taarifa kutoka Kigoma ambazo mtandao huu wa umezipata hivi punde zinadai  kuwa mwili wa mwanahabari  huyo umekutwa nje  kidogo na mkoa  wa Kigoma.
 
Kamanda  wa  polisi  wa mkoa wa Kigoma RPC Kishai amethibitisha  kutokea kwa  tukio  hilo na kuwa bado jeshi la  polisi  linaendelea na uchunguzi zaidi .

Mbunge wa  jimbo la Kigoma Zitto Kabwe pia amepata  kuzungumza na mtandao huu na kudai  kuwa ameguswa na kifo cha mtangazaji huyo na  kutaka  jeshi la  polisi kufanya uchunguzi wa kina  dhidi ya kifo  chake 

Pia Kabwe  ameeleza  jinsi ambavyo  mwanahabari  huyo  alivyoweza kuifanya kazi yake kwa jamii ya Kigoma kwa ufanisi zaidi na kuwa wakati mwingine yeye kama mbunge alikuwa akizunguka na mwanahabari huyo katika jimbo lake.

" Kweli  nimeguswa   sana na kifo  cha kusikitisha cha mwanahabari huyo nilimfahamu  vema kwa  utendaji kazi wake  ila nawapa  pole sana  waandishi  wote nchini kwa  msiba huu mkubwa .....na zaidi nitapata  kueleza mengi mara baada ya  uchunguzi"
Taarifa za awali  zilizotolewa na  Jeshi la Polisi wilayani Kakonko baada ya  kupotea kwa mwanahabari huyo zilisema kuwa Bw Ngumba alipotea  tangu January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi. Rukia Yunus kuwa anakwendwa Muhange senta wilayani Kakonko na kwamba hajarudi nyumbani hadi sasa.
 
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Muhange wanaendelea kumtafuta katika mapori ya kijiji hicho baada ya rafiki zake kueleza kuwa aliwaanga kuwa anakwenda kutafuta dawa msituni.
 
Bw. Issa Ngumba.
Aidha jeshi la polisi Wilayani Kibondo liliomba kampuni za mitandao ya simu anayotumia Bw Ngumba kusaidia kutambua simu zake zilipotumika kwa mara ya mwisho ili kurahisisha upatikanaji wake.
 
Akizungumza kwa njia ya simu, Mke wa Bw Issa Ngumba, Bi Rukia Yunus amesema kuwa wananchi walio wengi ambao walikuwa wakimtafuta maporini wamerudi kijiji hapo baada ya kumkosa.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger